Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:07

Waandamanaji Marekani wataka mchunguzi maalum dhidi ya Russia alindwe


Waandamanaji wakishinikiza Mchunguzi Maalum katika uchunguzi wa Russia kulindwa na serikali, Alhamisi Novemba 11, 2018.
Waandamanaji wakishinikiza Mchunguzi Maalum katika uchunguzi wa Russia kulindwa na serikali, Alhamisi Novemba 11, 2018.

Waandamanji kote nchini Marekani wanataka mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller anaye endesha uchunguzi unao husisha kitendo cha Russia kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016 kulindwa.

Mamia ya waandamanaji wamekusanyika mjini New York, eneo la Times Square, wakitaka Robert Muller kutoingiliwa kati katika kazi yake na kusisitiza kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Wanasema kuwa ni jukumu la serikali ya Marekani kumlinda mchunguzi huyo maalum wakati akiendelea kuchimbua madai ya Russia kuingilia kati kampeni ya Rais Trump ya 2016.

Katika jimbo la Chicago, Seneta wa Chama cha Demokrat Dick Durbin ameungana na mamia wa waandamanaji nje ya Jengo la Serikali Kuu.

Maandamano pia yameshuhudiwa nje ya ikulu ya Rais Donald Trump, Greensboro, North Carolina; Chattanooga, Tennessee, Las Vegas na sehemu nyingine mbalimbali nchini.

XS
SM
MD
LG