Shirika la habari la BuzzFeed News zilinukuu vyanzo viwili visivyo tajwa majina ambao ni maofisa wa vyombo vya usalama vya serikali kuu katika ripoti yake kwamba Trump alikuwa amemuamrisha wakili wake wa zamani, Michael Cohen, kusema kuidanganya Congress juu ya mkakati wa ujenzi wa jumba refu la Trump huko Moscow.
Hata hivyo, msemaji wa mchunguzi maalum Peter Carr amesema Ijumaa, “ maelezo ya BuzzFeed katika matamko mahsusi juu ya ofisi ya mchunguzi maalum, ikiwemo ufafanuzi wa makabrasha na uthibitisho uliopatikana na ofisi hii, kuhusiana na ushahidi uliotolewa na Michael Cohen katika Congress, sio sahihi.
Maoni hayo ni tamko ambalo ni nadra kutolewa na ofisi ya mwendesha mashtaka maalum katika kukosoa habari zinazo ripotiwa na vyombo vya habari.
Muda mfupi baada ya ofisi ya Mueller kulizungumzia hilo, Ben Smith, Mhariri mkuu wa BuzzFeed, alisema katika tamko lake kuwa alikuwa anaendelea kutetea habari zilizo andikwa katika mtandao wa habari wa shirika hilo na kumtaka “mwendesha mashtaka maalum kuweka wazi nini anacho kipinga katika ripoti hiyo.”
Ripoti hiyo ya BuzzFeed ilisababisha wakuu wawili wa kamati za Baraza la Wawakilishi (Congress) kutangaza kuwa watalichunguza suala hilo.