Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:44

Mwanajeshi Kenya alalamika aliadhibiwa badala ya kupewa tiba


Mkutano wa maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Africa nchini Somalia (AMISOM) na washiriki wengine wa kimataifa, Mogadishu, Somalia, Feb. 15, 2019. (O. Abdisalan/AMISOM)
Mkutano wa maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Africa nchini Somalia (AMISOM) na washiriki wengine wa kimataifa, Mogadishu, Somalia, Feb. 15, 2019. (O. Abdisalan/AMISOM)

Katika vita dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab nchini Somalia, Wamarekani wanafanya mashambulizi zaidi angani kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani.

Ripoti ya gazeti la Washington Post Mei 30, inaeleza kuwa upande wa ardhini, katika vizuizi vya usalama vilivyoko maeneo yenye jua kali na mabondeni kwenye vumbi jingi kuelekea majimbo mengi yaliyoko kusini mwa Somalia, wanajeshi wa Kenya, nchi iliyoko jirani, ndio ambao wanapigana takriban vita yote hiyo.

Mmoja wa wanajeshi hao ni Christopher Katitu, ni askari wa ngazi ya chini katika jeshi la ulinzi Kenya (KDF), ambaye ametumikia kwa miaka miwili kusimamia silaha ya kivita aina ya rashashi iliyoko katika handaki huko Kismayo, bandari ya Jiji hilo ambayo imesambaratishwa na mapigano ya silaha yanayoendelea mtaa kwa mtaa katika eneo hilo.

Na hivyo, pale al-Shabaab walipouwa takriban wanafunzi 150 katika chuo kikuu ambacho kiko upande wa pili wa mpaka eneo la Garissa, Kenya, Katitu alipelekwa kulinda mpakani mwa jiji hilo lenye mapigano katika kizuizi cha usalama cha barabara kuu, kwa mfululizo usiku na mchana.

Aina fulani ya msongo wa mawazo ulianza kujitokeza katika ubongo wake, tatizo ambalo hakuweza kulitambua. Ilikuwa sio tu vita – matatizo ya fedha yalikuwa yanaongezeka nyumbani, pia, na mkewe alikuwa amemkasirikia. Kwa kipindi cha muongo mmoja akitumikia jeshini, alikuwa hajawahi kupata ushauri nasaha.

Katika likizo fupi kutoka Garissa, Katitu alikuwa amechanganyikiwa. Lakini badala ya kupewa matibabu ya msongo wa akili unatokana na athari za vita, alifungwa jela na kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi wakati alipokuwa anajaribu kurudi na kujiunga na kikosi chake

Tangu Kenya ilipoingia katika vita nchini Somalia mwaka 2011, Marekani imeipa serikali ya Kenya zaidi ya dola za Marekani nusu bilioni kwa ajili ya kusaidia masuala ya ulinzi.

Msaada huo unatolewa bila ya kusisitiza kuwa sehemu ya msaada huo utumike kwa matibabu ya afya ya akili kwa askari wake, lakini jeshi la Marekani linawafundisha madaktari wa jeshi la Kenya juu tiba ya masuala ya afya ya akili.

Daktari Mkuu wa Jeshi la Kenya, George Ng’ang’a amesema : Iwapo kuna eneo moja tumesonga mbele ni afya ya akili.”

Lakini katika mahojiano na madaktari wa KDF, wataalam wa afya ya akili na darzeni ya askari wa zamani wa Jeshi la Kenya, taswira inajitokeza kuwa mfumo huo unapendelea kuwaadhibu kuliko kushughulikia afya ya akili za mamia wanajeshi wanaokabiliwa na tatizo la msongo wa akili.

Kitendo cha kulikosoa jeshi ni kosa, na ugonjwa wa akili ni nadra kujadiliwa ndani ya jeshi au katika jamii kwa ujumla.

Miaka minane ya operesheni za kijeshi ndani ya Somalia, mamia ya askari wa Kenya wameuawa na darzeni ya mashambulizi ya al-Shabaab yametokea katika ardhi ya Kenya, na mengine kuelekezwa kwa wanajeshi wa KDF.

Kenya ina wanajeshi 4,000 nchini Somalia, ambayo ni moja ya tano ya kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopelekwa nchini humo.

Jeshi la KDF linasema kuwa linatoa huduma ya ushauri nasaha, lakini Ng’ang’a amesema katika mahojiano kuwa KDF haina kumbukumbu zozote juu ya wagonjwa wa akili, au kutenga hospitali ya afya ya akili.

Hakuweza kubainisha ni wataalam wangapi wa saikolojia wameajiriwa na KDF.

Kikosi cha Jeshi la Marekani cha Africa Command kimesema kimejiandaa kusaidia kujenga jeshi la Kenya ambalo ni mshirika wake lenye weledi na uwezo kamili..

XS
SM
MD
LG