Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 17:10

Kenya, Ethiopia zakubaliana kutokomeza ugaidi na kuimarisha uchumi


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia) akiwa pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Jenerali Samson Mwathethe, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi mara baada ya kuwasili Ikulu ya Nairobi, Mei 7, 2018.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia) akiwa pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Jenerali Samson Mwathethe, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi mara baada ya kuwasili Ikulu ya Nairobi, Mei 7, 2018.

Kenya na Ethiopia wamekubaliana kuharakisha utekelezaji wa mkataba wenye hadhi ya kipekee kati ya nchi hizo mbili, ambao unatarajiwa kuwa na maslahi ya kiuchumi na kiusalama kwa raia wake.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Jumatatu Kenya na Ethiopia wamekubaliana kuanzisha Tume ya Ushirikiano, ambayo ni muundo wa ngazi ya juu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Rais Uhuru Kenyatta ameeleza kuwa mzunguko wa bidhaa na watu kati ya nchi hizo mbili umeboreshwa kutokana na ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani katika mji wa Moyale, Ethiopia.

Amesisitiza ratiba kamili itolewe na bidhaa zinazohitajika lazima ziweze kupatikana kwa maslahi ya wananchi wa nchi hizo kutokana na mahusiano haya maalum.

“Napenda kutoa wito kuwepo msukumo mpya wa kuhakikisha hili linatekelezwa kwa mafanikio, kwa kuweka ratiba iliyo wazi na upatikanaji wa bidhaa zote katika hatua ya utekelezaji wa mkakati wetu,” amesema Rais Kenyatta.

Rais alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa ushirikiano wa pande mbili katika Ikulu ya Kenya, baada ya kuwasili Abiy Ahmed ambaye anafanya ziara ya kiserikali.

“Tumefanya mazungumzo na kukubaliana kuangaza ushirikiano wetu wa kihistoria ambao mababu zetu waliujenga kwa ajili yetu. Tunayo fahari kwa yale tuliyokuwa tunayafanya kwa miaka mingi na lazima tuweze kufanikisha mengi zaidi,” amesema Abiy ambaye amechukuwa nafasi ya uwaziri mkuu mwezi wa April.

Viongozi hao wawili pia wamezungumzia utekelezaji wa makubaliano ya manunuzi ya umeme, ambapo Kenya itanunua 400 MW kutoka Ethiopia kila mwaka.

Ethiopia hivi sasa inakabia kumaliza mradi wa umeme wa Bwawa la Grand Renaissance ambao wanatarajia utawawezesha kukidhi mahitaji ya umeme ya eneo hilo.

Wakati Misri imepinga ujenzi wa mradi wa bwawa la kuzalisha umeme kwa sababu ya hofu kwamba utaathiri maporomoko ya maji, Sudan na Kenya tayari vimeeleza nia yao ya kutumia fursa iliyopo ya kununua umeme kutoka Ethiopia.

Rais Kenyatta na waziri mkuu Abiy pia wamezungumzia mkakati wa nchi hizo mbili katika kupambana na ugaidi ambapo wametoa kipaumbele cha kurudisha utulivu Somalia na kushinda vita dhidi ya Al Shabaab.

XS
SM
MD
LG