Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:30

Amisom yafanya tathmini ya shughuli zake nchini Somalia


Majeshi ya kulinda amani AMISOM nchini Somalia
Majeshi ya kulinda amani AMISOM nchini Somalia

Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika, AMISOM nchini Somalia linachukua hatua ya kutathmini hali halisi ya operesheni zake kwa miaka 11 nchini Somalia.

Imesema baada ya zoezi hilo itaufahamisha umma hali ilivyo katika eneo la vita upande wa mashariki mwa nchi hiyo ya Afrika, ilioko katika eneo la Pembe ya Afrika.

Tathmini hiyo itafanyika kwa kiasi cha mwezi mmoja na wakati mchakato huo ukifanyika, waandishi wa habari kutoka nchi zinazochangia majeshi watatembele kambi mbalimbali za jeshi hilo ambazo ziko maeneo mbalimbali nchini humo.

Zoezi hilo limeanza Mei 2, 2018, ambapo waandishi 14 kutoka Uganda watatembezwa katika baadhi ya maeneo hayo kwa siku tatu.

Msemaji wa AMISOM, Luteni Kanali Richard Omwega amewaambia waandishi wa habari walipowasili Mogadish, kuwa zoezi hili linakusudia kutoa tathmini ya uwepo wa majeshi hayo ya kigeni nchini Somalia.

Tunataka nyie waandishi mshuhudie kile kinachoendelea ili iwasaidie katika ripoti zenu jinsi hawa kaka na dada wanavyoendelea kujitolea nafsi zao na kulipa thamani kubwa ya maisha yao,” amesema.

Kuna makundi matano ya majeshi yaliotolewa na nchi mbalimbali ili kuchangia katika kupambana na kikundi cha itikadi kali cha al-Shabaab nchini Somalia. Inawahusisha; Uganda, Kenya, Burundi na Djibouti pamoja na Ethiopia.

Wakati wa kuwakaribisha waandishi hao, Kanali Omwega alisema kuwa waandishi watatembelea majimbo ambako majeshi ya nchi zao yanalinda amani.

XS
SM
MD
LG