Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:18

Msimamo wa Uganda juu ya kutafuta usuluhishi waikasirisha Rwanda


Rais Museveni (kushoto), Rais Kagame
Rais Museveni (kushoto), Rais Kagame

Wakati suluhisho la mgogoro kati ya Rwanda na Uganda ukiwa bado haujafikia mafanikio mvutano huu wa mpakani umeuweka mashakani uongozi mzima Kigali, na kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya vyombo vya usalama na forodha, walitarajia hatua tofauti kuchukuliwa kutokana na kufungwa mpaka.

Lakini wakati mgogoro huo ukiingia wiki ya tatu, Kampala imekuwa haionyeshi umuhimu katika juhudi yeyote ya kuingia katika mazungumzo ya usuluhishi na wala haijatoa mrejesho wowote kama ilivyokuwa Rwanda inategemea, kwa kudhibiti zaidi huduma za forodha na uhamiaji katika upande wa mipaka yake.

“Tunasubiri kuona vile watakavyo jibu. Tulidhani kuwa serikali ya Uganda itakuwa na umuhimu wa kutatua tatizo hili kwa haraka,” afisa moja wa juu wa uhamiaji wa Rwanda amesema.

Madai ya Kagame

Hivi karibuni Rais wa Rwanda Paul Kagame alidai kuwa chanzo cha mgogoro kati ya nchi yake na Uganda ulianza miaka 20 iliyopita wakati Uganda ilipotaka kuuangusha utawala wake.

Rais Kagame alisema mgogoro huo umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kutokana na Uganda kuunga mkono kundi la RNC.

Kundi hilo linaipinga serikali ya Rwanda na alidai kuwa Uganda inawatummia kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea au wanaoishi nchini Uganda.

Juhudi za usuluhishi

Baada ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kukutana na wote Rais Yoweri Museveni na Paul Kagame Machi 11, kwa kile wachambuzi wanachosema wanaamini ilikuwa ni juhudi ya kuzipatanisha nchi hizo mbili.

Ziara ya Kenyatta Uganda, Rwanda

Rais Uhuru alikuwa Uganda kwa ziara fupi ya kikazi. Viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na kieneo,” tamko la ikulu ya Entebbe lilieleza.

Gazeti la East African linaeleza kuwa tangu wakati huo limepata kujua kwamba katika “masuala mbalimbali ya kitaifa na kieneo” yaliyozungumziwa wakati wa mkutano wake na Kenyatta, Rais Museveni hakuwa na umuhimu wa kuzungumzia suala la mgogoro wake na Rwanda.”

Badala ya kuhamasisha juhudi za Rais Kenyatta katika kutafuta usuluhishi, hali nchini Kampala imegeuka kuwa ni ya kuhamasisha suala la idadi ya watu, hasa wafanyabiashara ambao wanafanya biashara mpakani, ukweli ambao Kigali imeweka vikwazo vya biashara dhidi ya Uganda, ikikusudia kuudhoofisha uchumi wa Uganda.

Shughuli za forodha Gatuna/Katuna

Tayari, shughuli za Forodha katika eneo la Gatun/Katuna zimezorota na kuendelea hivyo kwa nyakati zote, na magari tu madogo na baadhi ya mabasi machache yakipita mpakani.

Hadi Februari 28 wakati Kigali ilipotoa tamko lake likishauri raia wake wasisafiri kwenda Uganda na kuendelea kufunga baadhi ya sehemu za mipaka, ambayo imekuwa yenye shughuli nyingi katika eneo la uvukaji kati ya Uganda na Rwanda.

Waziri wa mambo ya nje

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ametoa tamko kali Machi 13 wakati mgogoro huo ukiingia wiki ya tatu.

“Rwanda imeanzisha mfumo wa kibali cha kusafirisha bidhaa nje kwa wale wenye nia ya kusafirisha bidhaa Uganda.

Huu ni utaratibu wa kiufundi na sio-kizuizi cha ushuru wa biashara. Lakini kiuhalisia, hiki ni kikwazo cha kibiashara katika ushirikiano wa biashara na Uganda,” Kutesa ameandika katika tamko hilo.

XS
SM
MD
LG