Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:55

Kagame amfukuza kazi Mkuu wa Usalama wa Nje


Rwanda
Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemfukuza kazi Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Nje, Brig Jenerali Francis Mutiganda ikiwa sehemu ya mabadiliko yaliofanyika katika jeshi la ulinzi la nchi hiyo, gazeti la Chimp Corps la Uganda limeripoti.

Kagame pia Ijumaa ameamrisha Luteni Kanali Emmanuel Rukundo kuhamishwa kutoka makao makuu ya Usalama wa Taifa wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) “kwa udhibiti zaidi.’

Sababu za kuwafukuza Mutiganda na Rukundo hazijaweza kufahamika.

Lakini inaripotiwa kuwa ni ishara ya kushindwa kwao kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Vyombo vya habari vimeeleza kuwa baadhi ya maafisa wamesema kuwa ingekuwa ni kwa sababu ya utovu wa nidhamu wangekuwa wamekamatwa.

Mutiganda alichukuwa wadhifa huo wa Usalama wa Nje kutoka kwa Dan Munyuza mwaka 2012.

Mutiganda inasemekana alikuwa ametayarishwa kushika wadhifa huo na Inspekta Jenerali wa RDF wa zamani, Jenerali Jack Nziza.

Maafisa walio zungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao wamesema mabadiliko hayo ambayo yamepelekea Mutiganda kuondoshwa kutoka katika nafasi yake, pia inawezekana yana mafungamano na uhusiano uliopo hivi sasa kati Rwanda na Uganda.

Uhusiano baina ya nchi hizo umezorota katika miezi ya hivi karibuni juu ya madai ya ujasusi na tuhuma za kuwa kila upande unasaidia waasi wa mwenzake.

​
XS
SM
MD
LG