Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:09

Serikali za kidikteta : Je, zimejifunza kutokana na historia ya Ufilipino?


Rais wa zamani wa Ufilipino Joseph Estrada
Rais wa zamani wa Ufilipino Joseph Estrada

Historia inatuambia kuwa ni wananchi wa Ufilipino walikuwa wanatumiana ujumbe wa simu katika kuhamasisha maandamano dhidi ya Rais Joseph Estrada, na kwa muda wa saa kadhaa “nguvu ya wananchi” ilimlazimisha Estrada kujiuzulu kutoka katika madaraka. Hilo lilitokea mwaka 2001.

Baada ya tukio hilo teknolojia imeweza kuleta simu zenye programu bora zaidi zinazojulikana kama "Smart phones" zinazoweza kuunganishwa na interneti, kumwezesha mtumiaji kupata habari mara moja na kuendeleza ukuaji wa mitandao ya kijamii.

Kwa nchi zenye udikteta, matokeo yake ni kuwa kumekuwa na mvutano wa kuzuia kile ambacho wananchi wao wanatakiwa kuona au kusikia, kuzuia upinzani – na kuzuia “nguvu ya wananchi” wao kuchukua madaraka.

Kuzuia habari, matumizi ya interneti

Kwanza ilianza na kuwazuia waandishi wa habari ambao walikuwa wanatishiwa, na ikawa ni vyombo vya habari ndio vinavyofungiwa,” anasema Arnaud Froger, mkuu wa deski la Afrika katika shirika la Waandishi Wasiokuwa na Mipaka.

Lakini hivi sasa serikali hizo zinazuia habari kutoenezwa kupitia interneti.

“Hilo ni jaribio la wazi kabisa la kutaka kunyamazisha sauti za wanaozikosoa serikali na kutoa taarifa muhimu ya mambo yanayohatarisha haki za jamii,” Froger ameiambia Sauti ya Amerika VOA.

Nchi za Kiafrika

Nchi kadhaa za Kiafrika, ikiwemo Uganda, Rwanda na Tanzania, zimeanza kutoza ushuru kwa wanaotumia interneti na mitandao ya kijamii – ikiwemo malipo yanayofanyika kutoka nje na ndugu wa familia- au zimeamrisha tovuti mbalimbali kulipa gharama za juu kupata leseni za kuendesha mitandao hiyo.

Sheria hizi zinazotumiwa na serikali zimepelekea mchezo wa paka na panya kufanyika kwa wale ambao wanataka kupambana na vizuizi hivi. Mtandao wa VPN umeendelea kutoa huduma kwa njia moja ya kuzuia mtumiaji wa internet kutoweza kujulikana jina lake na sehemu aliko wakati anatumia internet. Kwa kujibu mapambano hayo nchi kadhaa zimepiga marufuku mtandao huu.

Ukandamizaji nchi nyingine

Program zinazotumiwa na mitandao ya kijamii kwa mfano wa Telegram imepigwa marufuku Iran na nchi nyingine. Vietnam imeanzisha kikosi cha jeshi cha kupambana na vita vya mitandao ya kijamii kupambana na maoni “potofu” yanayotumwa kwenye mitandao hiyo na kukusanya habari za wale wanaoikosoa serikali. Saudi Arabia imewakamata dazeni ya watu wanaoeneza upinzani nchini humo. Wanaharakati ambao wako nje ya nchi akaunti zao za Facebook zimesitishwa kwa kuripoti madai ya uhalifu wa kivita unaofanywa na Saudi Arabia huko Yemen.

China imekuwa ikiruhusu kampuni za ndani ya nchi ambazo zinaendeshwa kwa kufuata sheria zilizowekwa bila ya kuzikiuka. Na huko Korea Kaskazini huduma ya interneti haipatikani kwa wananchi wote.

Wasiwasi uliopo katika nchi hizi

“Jambo hili limetuletea wasiwasi mkubwa,” amesema Froger.“Inaonekana kana kwamba nchi za Afrika ya kati, mashariki na kusini ziko katika mashindano ya kuzuia matumizi ya Interneti kwa jumla na hasa mitandao ya kijamii.

“Waandishi wa habari na wananchi wanaoripoti matukio kwa kweli wameathiriwa na amri hizi kwa kuwa mara nyingi wanatumia Facebook kuposti Makala zao mbalimbali na wanatumia Whatsapp kuwasiliana na vyanzo vyao vya habari.

Lakini ikiwa ni ishara ya namna gani watu wameendelea kuitegemea interneti na mitandao ya kijamii, hasira zao zimejitokeza kwa wingi kwa hatua za kisheria walizochukuwa na maandamano wanayofanya ambayo serikali za nchi zao wamekuwa wakijaribu kuyazuia.

Matukio ya hivi karibuni

Maafisa wa Uganda wanasema watafikiria mara nyingine ushuru uliowekwa kwa mitandao ya kijamii baada ya maandamano makubwa kufanyika wiki hii ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi na kupiga risasi hewani kuwatawanya waandamanaji hao.

“Mara nyingine baadhi ya mambo hufanikiwa,” Froger amesema. “Hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa, na maandamano yanaweza kufanyika katika mitaa mbalimbali.

Cameroon hivi sasa ni nchi ya kwanza Afrika kushtakiwa mbele ya mahakama ya kikatiba kwa hatua yake ya kuzuia internet.

Wakati mwengine kwa kulaani, kuonya na kuongeza ufahamu wa umma kunatosheleza kuishawishi serikali kuacha kuingilia kati mitandao ya kijamii.

XS
SM
MD
LG