Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:11

Uganda, Rwanda zaendelea kunyoosheana vidole


Rais Museveni na Rais Kagame
Rais Museveni na Rais Kagame

Maafisa wa Uganda wanadai Rwanda imetuma jeshi lake mpakani, huku mzozo wa kidiplomasia ukiendelea kufukuta baada ya Rwanda kufunga mpaka wake.

Msemaji wa polisi wa Uganda Fred Enanga, amewaambia waandishi wa habari, jijini Kampala, kwamba idadi ya maafisa wa polisi wa Uganda imeongezwa mpakani kwa usalama wa raia wa Uganda. Amesema kuwa Uganda haina sababu ya kutuma jeshi.

Tuhuma za Rwanda dhidi ya Uganda

Hata hivyo serikali ya Rwanda inaituhumu Uganda kwa kuhatarisha usalama wake.

“Tunasikitiko la Uganda kuwasaidia watu wenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) linalojulikana kwa jina la Rwanda National Congress of Kanyumba Nyamwasa," imesema.

Rwanda na Uganda zimekuwa zikizozana kwa muda sasa, kila upande ukiripotiwa kuwakamata au kuwafukuza raia wa jirani yake kwa madai ya kuhatarisha usalama.

Uhusiano wadorora

Wachambuzi wanasema kwamba uhusiano umeendelea kudorora, kila upande ukimtuhumu mwenzake kwa kukaribisha na kuwa rafiki wa wanasiasa au makundi yanayompinga jirani yake.

Kulingana na maafisa wa Uganda, wanajeshi wa Rwanda wameonekana Jumatatu wakipiga doria mpakani katika milima ya Mukaniga, Byumba, Buganza na karibu na mpaka wa Chanika wilayani Kisoro.

Mzozo kati ya Rwanda na Uganda umeendelea kuongezeka baada ya Rwanda kufunga mpaka wake na Uganda, ulioko mji wa Chanika Jumatano wiki iliyopita.

Taarifa ya awali ya Rwanda ilisema mpaka ulifungwa kwa sababu Rwanda ilikuwa ikikarabati kituo chake cha mpakani cha Gatuna.

Siku sita baada ya kufungwa mpaka

Siku sita baadaye, mpaka huo umeendelea kufungwa huku waziri msaidizi wa mambo ya nje wa Rwanda Balozi Olivier Nduhungirehe akitangaza marufuku kwa raia wa Rwanda kuingia Uganda.

“Tumewashauri raia wa Rwanda wasiingie Uganda kwa sababu hatuna uhakika juu ya usalama wao wakiwa huko. Kuna raia wengi wa Rwanda ambao wamekamatwa, kuteswa na kuzuiliwa na maafisa wa usalama wa Uganda. Hali imekuwa tete sasa ndio maana tunawazuia raia wetu kuingia huko”.

Pia amesema kuwa magari yamezuiliwa mpakani, harufu mbaya ya bidhaa zinazooza ikiwa imeenea katika eneo hilo.

Athari za kufungwa mpaka

Kati ya magari yanayozuiliwa kuvuka mpaka na kuingia Rwanda, 10 ni zenye namba za usajili za Rwanda, 49 kutoka Uganda, 37 kutoka Kenya na 9 kutoka Burundi.

Magari hayo yamebeba bidhaa kama maembe, samaki, mihogo, mafuta ya diesel na petrol miongoni mwa nyingine.

Kampuni ya mabasi kutoka Kigali kuelekea Kampala, yamesitisha usafiri, huku serikali ya Rwanda ikisisitiza wasafiri watumie mpaka wa Kagitumba ambao mamlaka ya Kampala inasema ni safari ndefu na hasara kwa wafanyabiashara.

Imetyarishwa na Mwandishi wetu, Kennes Bwire, VOA, Washington, DC

XS
SM
MD
LG