Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 07:01

Tanzania, Rwanda zaimarisha rekodi ya kupambana na ufisadi -TI


Jinsi Transparency International (TI) ilivyoonyesha ripoti yake kuhusu ufisadi duniani ya mwaka 2018
Jinsi Transparency International (TI) ilivyoonyesha ripoti yake kuhusu ufisadi duniani ya mwaka 2018

Shirika la kimataifa la Transparency  International (TI), Jumanne lilitoa ripoti inayoonyesha hali ya ufisadi duniani mwaka 2018. Mataifa ya Tanzania na Rwanda yaliorodheshwa kama yaliyofanya  vizuri  katika vita dhidi ya rushwa.

Rwanda ilitajwa kufanya vizuri zaidi kwa kuwa na pointi 56 ikiwa katika nafasi ya 48 wakati Tanzania ikiwa katika nafasi ya 99 kwa kupata pointi 36.

Ripoti hiyo pia imebaini kuwa Kenya ilishuka kwa pointi moja kutoka mwaka 2017, ambapo ilikuwa na pointi 28, huku mwaka jana ikiwa na pointi 27 na kushika nafasi ya 144 kati ya nchi 180.

Uganda ilipata pointi 26 na kuchukua nafasi ya 149. Burundi iko katika nafasi ya 170 huku Sudan ikiwa katika nafasi ya 172 ikiwa na pointi 16.

Transparency International hutumia vigezo ambapo sufuri ni alama ya nchi inayofanya vizuri zaidi huku mia moja ikiwa ndiyo nchi iliyozorota Zaidi katika Nyanja hiyo.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Ferreira Rubia, alisema kuwa jinsi demokrasia ilivyokita mizizi kwa baadhi ya nchi, ndivyo uwezekano wa nchi hiyo kufanya vyema katika orodha hiyo ya nchi fisadi zaidi duniani.

Hata hivyo, nchi kama Marekani, ambayo hutajwa kama iliyoimarika kidemokrasia, pia ilishuka rekodi tyake kutoka ilivyokuwa mwaka wa 2017.

Denmark na New Zealand ziliongoza kwa nchi zisizo na viwango vya juu vya ufisadi, lakini nchi fisadi zaidi ni pamoja na Somalia, Sudan Kusini na Syria.

Hizi ni nchi ambazo zimekuwa katika vita vya aina moja au nyingine, ikiwa ni ishara kwamba misukosuko ya ndani ya nchi inaathiri sana vita dhidi ya ufisadi, alisema mchambuzi wa masuala ya uchumi, Chrispus Yankeem katika mahojiano ya simu na Sauti ya Amerika siku ya Jumanne.

XS
SM
MD
LG