Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:24

Idara ya usalama Uganda yamwachia Raia wa Rwanda


Rais Paul Kagame (kushoto) na Rais Yoweri Museveni
Rais Paul Kagame (kushoto) na Rais Yoweri Museveni

Idara za usalama nchini Uganda imemwachia raia wa Rwanda ambaye alikamatwa huko mjini Mbarara.

Watu wa idara ya usalama waliokuwa na silaha walivamia nyumbani kwa Emmanuel Cyemayire Januari 5 kabla ya kumuamuru apande ndani ya gari lao ambalo lilielekea kule kusikojulikana.

Vyanzo vya habari nchini Uganda vimesema kuwa Mke wa Cyemayire baadae aliripoti kutoweka kwa mtu huyo katika kituo cha polisi cha Mbarara.

Askari hao baadae walisema kuwa hawakuwa wanamshikilia mtu huyo rumande.

Inaeleweka kuwa Cyemayire alikuwa amehojiwa na vyombo vya usalama kwa kuwa na mahusiano na idara za usalama ya Rwanda.

Maafisa wamesema Cyemayire anashukiwa kuwa alihusika katika vitendo vya ujasusi na kuwasumbua wakimbizi wa Rwanda wanaoishi Rwanda.

Muhtasari wa kijasusi uliotolewa asubuhi umepata habari kuwa Cyamayire alikuwa ameachiwa huru wiki hii.

Maafisa wa usalama wa Uganda walimchukua hadi mpakani Katuna,” amesema afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kujieleza kwa uhuru zaidi. “Hakuna tuhuma zozote zilizofunguliwa dhidi yake.”

Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa tukio hilo limekuja wakati Kampala na Kigali wanafanya juhudi kutafuta suluhisho katika suntafahamu iliyojiri katika kukamatwa kwa raia wa Rwanda nchini Uganda, kuhama kwa wapinzani, kusumbuliwa kwa wakimbizi kati ya mambo mengine.

Rais Museveni wiki hii amekutana na kiongozi mwenzake Rais Paul Kagame kuhusu suala hili.

Ugandan officials accuse the arrested Rwandan nationals of espionage, harassment of refugees and engaging in acts that threaten the country’s national security.

Maafisa wa Uganda wanawashutumu raia wa Rwanda waliokamatwa kwa kuhusika na ujasusi, usumbufu kwa wakimbizi na kujihusisha na mambo yanayo hatarisha usalama wa taifa wa nchi hiyo.

Lakini Rwanda inadai kuwa raia wake wanaokamatwa lazima wazuiliwe katika vizuizi vilivyo idhinishwa na waruhusiwe kuonana na ndugu, madaktari na kupatiwa huduma za ubalozi.

XS
SM
MD
LG