Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:28

Bei za hisa zaendelea kushuka Ulaya na Asia


Kampuni ya uchimbaji mafuta West Texas Intermediate (WTI) katika Jimbo la California.
Kampuni ya uchimbaji mafuta West Texas Intermediate (WTI) katika Jimbo la California.

Biashara kwenye Masoko ya fedha ya Ulaya imeshuka leo Alhamisi kukiwa na ongezeko la hofu ya kwamba uchumi wa dunia bado unakabiliwa na hatari ya janga la virusi vya corona.

Kipimo cha hisa cha Uingereza FTSE kimeshuka kwa kishindo kwa asilimia 2.2 katikati ya siku ya mauzo, wakati kile cha Paris CAC-40 kilikuwa chini wakati wa mauzo kwa asilimia 1.8 na cha Frankfurt Dax kiliporomoka kwa asilimia 1.5.

Hisa zilianza kuuzwa kwa haraka Alhamisi bara la Asia, na kusababisha kipimo cha hisa cha Tokyo Nikkei na kile cha Sydney S&P/ASX vyote kupata hasara ya asilimia 1.7 wakati wa kumaliza mauzo. Masoko ya hisa ya Hong Kong, Seoul, Shanghai na Taipei yalipata hasara kubwa.

Wawekezaji wanaonekana kuvunjika moyo kutokana na tahadhari iliyotolewa Jumatano na Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani Jerome Powell, kuwa hali ya kudorora hivi sasa kwa uchumi imesababishwa na mlipuko wa COVID-19 ulimwenguni na utaendelea kwa muda mrefu katika siku za usoni.

Nchini Marekani biashara kwenye masoko ya fedha, kipimo cha Dow Jones kilikuwa kimeshuka kidogo kimauzo, wakati S&P 500 na Nasdaq yalikuwa katika wigo chanya wa biashara, wakati soko la Wall Street Alhamisi likionyesha mwanzo wenye biashara mchanganyiko.

Wakati bei ya hisa inaendelea kuyumba, bei ya mafuta inapanda. Bei ya mafuta ghafi ya kipimo cha Marekani, West Texas Intermediate, inauzwa dola za Marekani 26.37 kwa pipa, kikiwa juu kwa asilimia 4.2, wakati bei ya mafuta ghafi cha Brent ambacho ni kipimo cha kimataifa, inauzwa kwa dola 30.28 kwa pipa, ikiwa juu kwa asilimia 3.7.

XS
SM
MD
LG