Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 11:09

Marekani : Azimio la kulinda haki ya matumizi ya intaneti Afrika lawasilishwa


Karen Bass
Karen Bass

Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Mambo ya Nje katika Baraza la Wawakilishi Karen Bass (Mdemokrat wa California) amewasilisha azimio linalozitaka serikali za Afrika kulinda na kuhamasisha haki za kibindamu kupitia uhuru wa intaneti na kuwaunganisha kidijitali raia wa nchi zote za Afrika.

“Kuzuia au kuminya haki ya kushiriki katika mitandao ya jamii inavunja haki za uhuru wa kujieleza, inapunguza fursa za kiuchumi, na kukandamiza ushiriki wa kisiasa,” amesema Mwakilishi Bass.

“Serikali nyingi za nchi za Kiafrika zimeendelea kueleza kuwa maudhui yaliyoko katika intaneti ni ‘habari feki’ ikiwa ni msingi wa kuzuia habari kusambaa wakati wa matukio ya maafa, mashambulizi ya kigaidi na taharuki za kijamii.

Serikali za Kiafrika pia zimekuwa zikiwabughudi na kuwaweka kizuizini waandishi, watoa taarifa, mabloga na wafanyakazi wa vyombo vya habari wakati wakitekeleza wajibu wao katika kusambaza habari kwa wananchi.

Mwakilishi huyo amesema mara nyingi fursa za kutumia intaneti zinabanwa wakati wa uchaguzi wa kisiasa, maandamano na upingaji wa namna yoyote.

Hizi hasa ni nyakati ambazo kuweza kupata habari, uhuru wa habari na ushiriki wa kisiasa ni muhimu katika mchakato wa kidemokrasia na utawala wa kisheria.

Ameongeza kuwa :"Lazima tulaani matumizi ya intaneti kama ni chombo cha ukandamizaji dhidi ya jamii na kuzitaka serikali kushirikiana na jumuia za kiraia na vyombo vya habari kuhakikisha utamaduni thabiti ambao raia wote wanapata habari bila ya kizuizi chochote."

Azimio hili linalaani vizuizi au hujuma dhidi ya intaneti kupitia njia au hali yoyote, ikiwemo kuzimwa kwa intaneti kikamilifu, “kuharibu mifumo ya intaneti, kudhibiti njia za matangazo, kutoza kodi kubwa, na kuzuia huduma na vifanyia kazi.

Pia imeonya dhidi ya matumizi ya teknolojia kutoka nchi nyingine zinazotumia mashambulizi ya kimitandao kwa ajili ya udukuzi na udhibiti, kuingilia faragha na kujasusi dhidi ya washindani wao.

XS
SM
MD
LG