Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:34

Uganda yaanzisha ushuru kwa wanaotumia Facebook, WhatsApp


Sheria mpya nchini Uganda itawalazimisha watu wanaotumia mitandao ya jamii kuilipia iwapo wanataka kutumia mitandao kama vile Facebook na WhatsApp.

Sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa Julai 1, inawataka wanaotumia mitandao hiyo kulipia shilingi 200 za Uganda. Bunge la Uganda liliidhinisha muswada huo siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uganda raia pia watalipia miamala yote ya kibiashara inayofanyika kupitia simu za mkononi, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa asilimia 1 ya thamani yake.

Rais Yoweri Museveni mwezi Mei alisema kuwa mitandao ya jamii hutumika zaidi kwa "udaku".

"Ni sehemu tu ya majaribio ya kufinya uhuru wa kujielezea ," Mwana Blogi Rosebell Kagumile ameliambia shirika la habari la Reuters.

Kwa upande wa Kenya waandishi wa habari na wamiliki wa blogi nchini Kenya wamepata ushindi wa kisheria katika mapambano yao dhidi ya sheria za mitandao ambazo wanasema zinaondoa uhuru wa kujieleza na kuhatarisha uhuru wa mamilioni ya Wakenya ambao wanatumia mitandao kutoa maoni yao.

Jaji Chacha Mwita, wa Mahakama ya Juu Jumanne alivizuia vifungu 26 vya sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta na uhalifu wa mitandao, ambayo Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameipitisha kuwa sheria mapema mwezi May.

Kenyatta amesema sheria hiyo itawalinda Wakenya na kuwahakikishia usalama na utulivu wa matumizi mapana ya mitandao ya mawasilian

Lakini wakosoaji wanadai kuwa imevunja Katiba ya Kenya na kukandamiza uhuru wa kujielezea pamoja na haki ya faragha ya mtu na umiliki.

Jumuiya ya Wanablogi nchini Kenya, ambao ni ushirika wa kutengeneza maudhui ya kidigitali wakiongozwa na Mwenyekiti wao Kennedy Kachwanyawalipeleka suala hilo mahakamani wakieleza kuwa katazo hilo litawazuilia, linavunja, linakandamiza na kutishia haki mbali mbali za binadamu na msingi wa tangazo la haki za binadamu kitu ambacho hakikubaliki chini ya kifungu cha 24.”

Kifungu cha 24 kinasema kuwa uhuru hauwezi kuzuiliwa ila tu ikiwa kufanya hivyo “kunahalalishwa na jamii iliyo na uwazi na demokrasia.

XS
SM
MD
LG