Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 22:49

Serikali ya TZ yashinda kesi dhidi ya wanablogi


Rais John Magufuli wa Tanzania.
Rais John Magufuli wa Tanzania.

Serikali ya Tanzania, Jumanne ilishinda kesi dhidi ya wanablogi na wanaharakati waliokuwa wanapinga utekelezaji wa kanuni mpya zinazowataka wamiliki wa mitandao kujiandikisha serikalini na kuwataja wafadhili wao.

Mapema mwezi huu (Mei), asasi sita za kiraia ziliwasiilisha hoja mahakamani inayotaka kanuni hizo zisitishwe kwa muda. Wanaharakati wameushutumu uamuzi huo wa mahakama kuwa ni shambulizi dhidi ya uhuru wa kujieleza.

Kanuni hizo mpya zinawataka wamiliki wa mitandao kulipa ada ya hadi dola $900 za Kimarakani, kutoa habari za wajasiriamali, uraia wa wamiliki, tajiriba ya wafanyakazi kati ya mengine.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, watakaokiuka kanuni hizo huenda wakafungwa jela kwa miezi 12, kupigwa faini ya shilingi milioni tano au adhabu zote mbili.

Tayari wamiliki wa mitandao na tovuti mbalimbali wameanza kusitisha huduma zao kwa kuhofia kukamatwa.

Baadhi ya wanaharakati wanamshutumu rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli, na kusema kuwa utawala wake umechukua hatua hiyo kwa sababu unaogopa kukosolewa.

Magufuli aliingia mamlakani mwaka wa 2015 kwa ahadi kwamba angeharakisha juhudi za kuimarisha uchumi na kukabilina na ufisadi nchini humo.

XS
SM
MD
LG