Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:59

Yemen : Mapigano mapya kati ya serikali na Wahuthi yaua watu 111


Wafanyakazi wakikagua jengo la Makumbusho ya Taifa lililoharibiwa kutokana na vitae National kusini Magharibi ya mji wa Taiz, Yemen Mei 26, 2021. Picture taken May 26, 2021. REUTERS/Anees Mahyoub
Wafanyakazi wakikagua jengo la Makumbusho ya Taifa lililoharibiwa kutokana na vitae National kusini Magharibi ya mji wa Taiz, Yemen Mei 26, 2021. Picture taken May 26, 2021. REUTERS/Anees Mahyoub

Mapigano kati ya waasi na wapiganaji wa serikali ya Yemen yameua watu wasiopungua 111 katika jimbo la Marib mnamo siku tatu, vyanzo vya habari vya serikali vimesema, kufuatia mashambulizi mapya yanayofanywa na Wahuthi. 

Waasi wa kikundi cha wahuthi chenye mafungamano na Iran wameongeza juhudi zao za kuteka Marib,ngome ya mwisho inayoshikiliwa na serikali huko kaskazini mwa Yemen, na tangu mwezi Februari, mauaji yamesababisha vifo vya mamia ya watu katika pande zote mbili, limeripoti shirika la habari la AFP.

Mapigano kati ya siku ya Alhamisi na Jumapili yameua wafanyakazi wa upande wa serikali 29 na waasi wasiopungua 82, vyanzo vitatu vya serikali vimeliambia shirika la habari la AFP. Wapiganaji wa waasi hawajathibitisha idadi hiyo ya vifo.

Maafisa wa serikali ya Yemen wamesema kuwa tangu Alhamisi, Wahuthi walifanya mashambulizi ya nguvu kutoka upande wa kaskazini, kusini na magharibi, lakini hawakufanikiwa kuingia katika ngome za ulinzi za serikali ambazo ziliimarishwa na mashambulizi ya angani yaliofanywa na ushirika wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia.

Kudhibiti jimbo lenye utajiri wa mafuta la Marib kutawapa nguvu Wahuthi kuweza kuwa na nafasi ya kufanya mazungumzo ya amani, lakini vita vimeongeza hofu ya kuongezeka kwa janga la kibinadamu, wakati wananchi wengi wa Yemen wakikimbia kutoka jimbo hilo wakiepuka mapigano katika maeneo mengine na nchi hiyo.

FILE - Mapigano yanaendelea Yemenl kati ya Ushirika wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi Jimbo la Marib, Machi 5, 2021.
FILE - Mapigano yanaendelea Yemenl kati ya Ushirika wa majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi Jimbo la Marib, Machi 5, 2021.

Vita vya Yemen vimeanza mwaka 2014 wakati Wahuthi walipouteka mji mkuu Sanaa, na kuibua Muungano wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia kuingilia kati kuisaidia serikali mwaka uliofuatia.

Wakati Umoja wa Mataifa na Washington zikishinikiza kumalizika kwa vita hivyo, Wahuthi wanadai kufunguliwa uwanja wa ndege wa Sanaa, uliofungwa chini ya kizuizi cha Saudi Arabia tangu mwaka 2016, kabla ya kusitishwa mapigano yoyote au mazungumzo.

Pamoja na mapigano ya umwagaji damu huko Marib, Wahuthi pia wameanza kutumia ndege zisizokuwa na rubani aina ya droni kushambulia na makombora katika maeneo ya Saudi Arabia, ikiwemo viwanda vya mafuta.

Mwezi huu mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen anayemaliza muda wake Martin Griffiths ameliambia Baraza la Usalama kuwa juhudi zake binafsi katika kipindi cha miaka mitatu kumaliza vita “hazikufanikiwa.”

Vita hivyo vimeua maelfu ya watu na kuwafanya asilimia 80 ya wananchi wa Yemen kutegemea misaada katika kile UN imekiita ni mgogoro mkubwa kuliko yote wa kibinadamu.

Chanzo cha Habari

XS
SM
MD
LG