Umoja huo unasema maisha katika taifa hilo linalokumbwa na vita ni mabaya ziadi na kwamba watoto wanakufa.
Zaidi ya mataifa 100 na wafadhli wanashiriki kwenye mkutano huo ambao kwa sehemu kubwa unafanyika kupitia mtandao na kufadhiliwa na Sweden na Uswizi.
Mkutanio huo unafanyika wakati Wahouthi wa Yemen wakizidisha mapigano huku wakijaribu kuchukua udhibiti wa jimbo la mwisho la kaskazni linaloshikiliwa na serikali la Mirbid.
Mwaka wa 2019 UN na washirika wake walipokea dola bilioni 1.9 kiasi cha nusu ya fedha walichohitaji, lakini msaada huo ukapunguka sana mwaka 2020 kutokana na janga la Corona pamoja na kuporomoka kwa uchumi duniani.