Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:20

Maafisa 2 wa polisi wakutwa na hatia, wahukumiwa kifo Kenya


Polisi nchini Kenya wakipiga risasi hewani wakati wa maandamano Novemba 17, 2017.
Polisi nchini Kenya wakipiga risasi hewani wakati wa maandamano Novemba 17, 2017.

Jaji mmoja nchini Kenya Jumatano amewahukumu maafisa wawili wa polisi adhabu ya kifo kwa kumuuwa mfanyakazi mwenzao na raia wawili mwaka 2014.

Uamuzi huo ni dalili mpya kuwa serikali inachukua hatua kali kukabili ukatili unaofanywa na polisi baada ya miaka kadhaa ambayo raia na vikundi vya haki za binadamu vimekuwa vikiwatuhumu polisi kwa kutumia nguvu za ziada lakini maofisa hao mara chache wameshtakiwa na kwa sehemu kubwa hawaadhibiwi.

Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imesema kuwa itapambana na vitendo vya kuzuia sheria isifuata mkondo wake wakati ambao pia imewakamata baadhi ya maafisa wa umma wa juu walioshtakiwa kwa ufisadi.

Mamlaka iliyo huru inayosimamia utendaji wa polisi (IPOA) amesema katika tamko lake uchunguzi wake umegundua kuwa maafisa hao Benjamin Changawa na Stanley Okoti walimuuwa mfanyakazi mwenzao , Joseph Obongo, na ndugu wawili wa askari huyo alieuwawa, akisema walikuwa wameshukiwa ni wezi. Obongo alikuwa ni mlinzi wa mbunge.

Mamlaka hiyo imesema Mkurugenzi wa Waendesha Mashtaka wa serikali waliichukuwa kesi hiyo baada ya IPOA kushauri kuwa maafisa hao washtakiwe kwa kosa la mauaji. Walikuwa wamehukumiwa mwezi Novemba, ni kesi ya tatu inayotokana na uchunguzi uliofanywa na IPOA.

Watuhumiwa hao walikuwa hawakabiliwi na hatari yoyote hata iwafanye watumie nguvu za ziada kuwauwa watu wasiokuwa na hatia kwa kwa mujibu wa wajibu wao.

XS
SM
MD
LG