Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:17

Muswada wa kubadilisha tarehe ya uchaguzi Kenya wagonga ukuta


Bunge la Kenya.
Bunge la Kenya.

Wabunge wa Kenya, Jumatano walishindwa kupitisha muswada uliokusudiwa kuifanyia katiba marekebisho, kwa nia ya kubadilisha tarehe ya uchaguzi mkuu. Hoja iliyokuwa imewasilishwa bungeni, ilitaka tarehe hiyo ibadilishwe kutoka mwezi Agosti, hadi mwezi Desemba.

Lakini muswada huo haukufua dafu baada ya kutopata idadi ya wajumbe inayo hitajika ili kuupigia kura.

Mapendekezo hayo yalikuwa yamewasilishwa na mbunge wa chama cha upinzani, Ford Kenya, Chris Wamalwa.

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, akizungumza wakati wa kikao cha Jumatano, alisema muswada huo haungepigiwa kura kwa sababu haukuungwa mkono na wabunge wa kutosha kama inavyo takikana na katiba.

Baada ya hesabu ya waliokuwepo bungeni kufanywa, spika huyo alitangaza kwamba kulikuwa na wabunge 187 na ili hali idadi ya wabunge waliohitajika kupitisha muswada wanatakiwa wawe 233, ili mchakato huo uendelee.

Haya yanajiri huku msukumo kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na Wakenya wa kawaida ukishika kasi, kutaka kufanyike kura ya maamuzi kwa lengo la kubadilisha katiba ya taifa hilo la Afrika Mashariki, katika kile kinachotajwa na wadau kama njia mojawapo ya kutatua matatizo ya kisiasa na kijamii yanayo ikabili nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG