Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:13

Melania Trump kuzuru Kenya Oktoba


Melania Trump akizungumza na wake wa marais wanaohudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 26, 2018.
Melania Trump akizungumza na wake wa marais wanaohudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 26, 2018.

Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump, atafanya ziara ya nchi nne za Afrika, mwezi Oktoba, ikiwemo Kenya.

Ziara hiyo itakayo anza Oktoba mosi itamchukua Melanie Trump pia katika nchi za Ghana, Malawi na Misri.

Alitangaza nchi hizo katika mkutano na wake wa marais wanao hudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Alisema nchi hizo “zenye kupendeza na zilizo kuwa tofauti,” zimechaguliwa kwa sababu “zimekuwa zikifanya kazi bega kwa bega na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID) na washirika wetu ili kupata mafanikio makubwa katika kutatua baadhi ya changamoto kubwa katika nchi hizi.”

Katika mkutano huo Bibi Trump alitambua uwepo wa Bi Margareth Kenyatta,mke wa rais wa Kenya na kusema “ilikuwa ni heshima kubwa kukupokea wiki chache zilizopita katika White House.”

“Huko Kenya, USAID inafanya kazi kwa kushirikiana katika programu mbalimbali, ikiwemo ya elimu ya awali ya watoto, kuhifadhi mazingira ya wanyama pori na kujikinga na Virusi vya Ukimwi,” Trump amesema.

Nchini Ghana, programu za USAID zimeangazia huduma za afya na inasaidia juhudi zinazoendelea kupanua huduma hizo na ubora wake kwa mama na mtoto mchanga anayezaliwa, na kuwaelimisha kina mama na watoto wadogo juu ya umuhimu wa lishe bora,” amesema.

“Huko Malawi, USAID imeweka mfano kwamba elimu ni moja ya vitu muhimu katika kupambana na umaskini na kuboresha maisha ya watu,” amesema Melania.

“Kituo changu cha mwisho, kitakuwa Misri, na kuangazia juu ya miradi ya utalii na hifadhi ya mazingira, lakini najua kuwa kupitia USAID, tumefanya kazi na wananchi wa Misri kuendeleza mazingira bora ambapo makundi yote katika jamii – wakiwemo wanawake na watu wachache wa dini nyingine, wanaweza kuishi maisha yenye tija na afya bora,” amesema.

Ukweli ni kuwa programu ya USAID imesaidia moja kwa moja katika kupunguza viwango vya vifo vya watoto na kina mama, imeboresha uwezo wa watu kujua kusoma mapema mashuleni na kuhuisha na kuhifadhi maeneo ya kihistoria ambayo ni muhimu kwa utalii wa Misri.

XS
SM
MD
LG