Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:10

Mawakili Kenya wakimbilia mahakamani kupinga ushuru


Bunge la Kenya
Bunge la Kenya

Muungano wa mawakili nchini Kenya umeishitaki serikali mahakamani kwa kuweka ushuru mpya kwa matumizi ya internet.

Mawakili wanasema kwamba ushuru huo unakiuka haki za msingi za binadamu na uhuru wa kujieleza.

Kesi ya mawakili

Muungano wa mawakili nchini Kenya, unapinga kile wanasema kwamba kodi ya internet ya asilimia 15 ni hatua za kubana uhuru wa kujieleza na haki ya kupata habari, mambo ambayo ni haki za kibinadamu na kwamba sheria nzima ya fedha ya mwaka 2018, ilipitishwa na bunge bila kufuata sheria zilizopo.

Mawakili wanasema kwamba rais Uhuru Kenyatta alikiuka sheria kulingana na kifungu cha sheria namba 115(1) (b), aliposaini sheria ya fedha ya mwaka 2018.

Mawakili wanataka mahakama kufutilia mbali sheria hiyo na kuzuia serikali kuitekeleza wakisema kwamba ushuru wa asilimia 15 kwa huduma za simu na internet utawanyima wakenya wengi haki ya kupata huduma za internet na hivyo kuwazuia kupata habari, jambo litakalochangia wao kutengwa na ulimwengu.

Gharama ya kupiga simu nayo itapanda kutokana na ushsuru huo.

Wakili George Kithi hata hivyo anasema kwamba huenda maombi ya muungano wa mawakili yakakosa kusikilizwa.

“Mahakama inaonekana haina uharaka wa kusitisha ushuru huo kwa sababu zizle kesi za kwanza ambazo zilienda, kama ushuru wa VAT ya 16%, mahakama haikutoa amri. Inaonekana kama mahakama haitaki kuingilia maswala ya bunge” amesema wakili George kithi.

Mwanaharakati Okiya Omtata

Mkuu wa sheria, bunge na mkuu wa idhara ya kukusanya ushuru Kenya, KRA wanatakiwa mahakamani kujibu kesi hiyo ambayo sasa mwanaharakati Okiya Omtata anataka ijumulihswe pamoja na kesi aliyoasilisha awali, kupinga mapendekezo yote ya nyongeza ya ushuru.

Maapendekezo ya ushuru yaliasilishwa na rais Uhuru Kenyatta, kujadiliwa na bunge, kupitishwa na baadaye kusainiwa na rais Uhuru na kuwa sheria.

Kulingana na mwanaharakati Okiya Omtata, huduma nyingi za serikali zinapatikana kwa mtandao na kwamba hatua ya kuongoza ushuru wa internet itawanyima wakenya wengi haki ya kupata huduma hiyo kutokana na gharama.

Omtata badala yake anapendekeza sserikali kuongeza ushuru kwa vitu za starehe kama pombe na magari.

“Ushuru ambao wanatozwa na wakenya sasa imepita kipimo. Imeanza sasa kuwa kama ni kuhujumu wakenya kwa njia ambazo zinawazuia kulinda mali yao. Huu ushuru ni sawa na kunyang’anya watu mali yao. Kwa kesi yangu nataka hiyo sheria ya fedha ya mwaka 2018 iharamishwe na mambo ya ushuru yaweze kufuatiliwa kwa misingi ya kikatiba”amesema Okiya Omtata.

Tetesi za raia na wimbo wa kura ya maoni

Serikali ya Kenya imekosolewa sana na raia wake, kutokana na ushuru mpya ambao wengi wanasema utachangia pakubwa katika kuongezeka kwa gharama ya maisha.

Serikali kwa upande wake imejitetea kwamba ushuru huo utasaidia katika ujenzi wa taifa.

Nyongeza ya ushuru, imepelekea baadhi ya Kenya kutaka kura ya maoni ili kuifanyia katiba marekebisho kwa lengo la kupunguza mzigo wa kuwalipa viongozi wa kisiasa, na kubana matumizi ya fedha.

Imeandikwa na Kennes Bwire, sauti ya Amerika, Washington DC.

XS
SM
MD
LG