Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:23

Wakenya wawili wakiri kusafirisha madawa ya kulevya


Kutoka kushoto : Baktash Akasha, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha na Vijaygiri Goswami wakiwa Mombasa, Kenya, Feb. 17, 2015.
Kutoka kushoto : Baktash Akasha, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha na Vijaygiri Goswami wakiwa Mombasa, Kenya, Feb. 17, 2015.

Ndugu wawili wanaotuhumiwa na waendesha mashtaka wa Marekani kwa kuwa vinara wa moja ya uhalifu wa kifamilia uliopewa jina la taasisi ya Akasha, wamekiri kosa linalotokana na tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya kuja Marekani, Jumatano, huko New York.

Baktash Akasha, 41, na ndugu yake Ibrahim Akasha, 29, kila moja alikiri kosa mbele ya Jaji wa Mahakama ya Wilaya Marekani Victor Marrero huko Manhattan kwa mashtaka saba yanayo wakabili, ikiwemo kusambaza madawa ya kulevya aina ya heroin na methamphetamine na kula njama za kuingiza madawa hayo nchini Marekani, kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakama.

Mashtaka hayo yana adhabu ya chini ambayo ni kifungo kisicho pungua miaka kumi jela na adhabu ya juu ni kifungo cha maisha.

George Goltzer, wakili wa Baktash Akasha, alikataa kutoa maoni yake. Wakili wa Ibrahim Akasha hakuweza kupatikana wakati huo.

Kesi hiyo inatokana na uchunguzi uliofanywa na Idara ya kuzuia madawa ya kulevya ya Marekani ndani ya kikundi cha Akasha, ambacho vyombo vya usalama vya Marekani vimeeleza kuwa ni walanguzi wakuu wanaohusishwa na mashamba ya mmea aina ya poppy huko Afghanistan, unaoleta madawa hayo katika miji ya Ulaya na Marekani.

Ndugu hao walisafirishwa kutoka Kenya kuja Marekani Januari 2017 wakiwa pamoja na Gulam Hussein, raia wa Pakistani aliyeshtakiwa kwa kuongoza mtandao wa madawa ya kulevya, na Vijaygiri Goswami, mfanyabiashara raia wa India ambaye anatuhumiwa kwa kusimamia biashara ya madawa ya taasisi ya Akasha.

XS
SM
MD
LG