Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:26

Washukiwa wa Mihadarati Kenya Wakutwa na Kilo 15 za 'Heroine' na 18m/-


Maafisa wa usalama Kenya
Maafisa wa usalama Kenya

Maafisa wa Polisi Mombasa wamewakamata watu 4 wanaoshukiwa kujihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya katika eneo la Pwani ya Kenya.

madawa ya kulevya
madawa ya kulevya

Waliokamatwa wamepatikana na kilo 15 za mihadarati aina ya 'Heroin' pamoja na shilingi milioni 18 pesa taslimu za Kenya ambazo ni sawa na dola 100,018.

Mwandishi wa VOA amesema kuwa watu hao wamekamatwa baada ya polisi kufanya msako mkali ambao ulifanikisha kuwakamata watu wanne wengine, raia wa kigeni.

Kati ya hao waliokamatwa wawili ni raia wa Afrika Kusini na wengine ni raia wa Ushelisheli ambao walikuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na polisi wa kimataifa (Interpol). Amesema watu hao tayari wamesafirihswa na kurejeshwa nchini kwao.

Akitoa taarifa kuhusu kukamatwa kwa watu hao Mkuu wa polisi wa eneo la Pwani Nelson Marwa amesema kuwa waliokamatwa katika msako wa jana usiku ni pamoja na Swaleh Yusuf Ahmed , mkewe Asma Abdala Ahmed na shemeji yake Farida Omar.

Mbali na dawa hizo ambazo zilikuwa zimefichwa kitongoji kimoja mjini Mombasa washukiwa walipatikana na shilingi 30,000/- ambazo ni sawa na dola 300 zikiwa katika sarafu na kwenye magari mawili.

Mda mchache baada ya maafisa wa polisi kuwafahamisha wanahabari washukiwa hao walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Kwa mujibu wa Marwa takriban vijana laki 5 katika eneo la Pwani ni watumiaji wa dawa za kulevya suala ambalo amesema linahitaji kushughulikiwa kwa kasi.

Amewaonya wanasiasa kutoingiza siasa katika jambo hilo na badala yake kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na uovu huo.

Vita dhidi ya walanguzi wa mihadarati vimeshika kasi katika mataifa ya Afrika Mashariki hasa Kenya na Tanzania, ambapo dunia imeshuhudia kukamatwa kwa ndugu wawili ambao ni watoto wa anayedaiwa kuwa mlanguzi wa dawa za kulevya aliyeuawa nchini Uholanzi, Ibrahimu Akasha na sasa wanawe wanakabiliwa na mashtaka ya madawa Marekani.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Liberty Adede, Kenya

XS
SM
MD
LG