Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Kimbunga Hinnamnor chasababisha huduma za masomo na usafiri kusitishwa China


Mtu akiwa katika baskeli ya tairi moja katika bonde la Mto Huangpu wakati Kimbunga Hinnamnor kikaribia Shanghai.
Mtu akiwa katika baskeli ya tairi moja katika bonde la Mto Huangpu wakati Kimbunga Hinnamnor kikaribia Shanghai.

Miji ya mashariki mwa China imesitisha huduma ya feri na masomo na safari za ndege zimefutwa nchini Japan Jumapili wakati kimbunga Hinnamnor, ambacho kina nguvu kubwa  mwaka huu duniani,  kimepiga kuelekea kupita Taiwan na Korea Kusini na Kaskazini  kikiwa na upepo mkali sana  na mvua nyingi.

Shanghai imesitisha huduma za feri na kupeleka zaidi ya maafisa polisi 50,000 kusaidia shughuli za uokoaji na kuelekeza magari upande mwingine mbali na maeneo hatari. Kitovu cha biashara cha mashariki cha Wenzhou kiliamuru shule zote kufungwa Jumatatu.

Hinnamnor kimetabiriwa kusogea polepole kuelekea kaskazini hadi bahari ya East China ikiwa na upepo wenye kasi ya kilomita 175 kwa saa, kulingana na kituo cha Ufuatiliaji Hong Kong.

Shughuli za kuwaondoa watu na kufutwa kwa safari za ndege zimeamriwa kufanyika katika kisiwa cha Okinawa kusini mwa Japan. Kimbunga hicho pia kinatarajiwa kuleta mvua kubwa katika Rasi ya Korea, kukiwa na uwezekano wa kutokea mafuriko.

Kituo cha taifa cha hali ya Hewa China kimetoa tahadhari ya manjano ya kimbunga saa nne asubuhi Jumapili kwa saa za huko, na kuonya kuwa mvua kubwa zitapiga kaskazini mashariki mwa Zhejiang, Shanghai na kisiwa kinachojitawala cha Taiwan.

Meli ziliarifiwa kurejea bandarini ili kujilinda na upepo, na kituo hicho pia kiliwasihi watu kuepuka mikusanyiko mikubwa ndani na nje ya nyumba.

Nchini Japan, kimbunga kilipiga Okinwa na visiwa vya karibu kwa mvua kubwa na upepo mkali sana, na kutishia mafuriko na kusimamisha zaidi ya safari za ndege 100 zinaingia katika visiwa hivyo na sehemu za kisiwa kikuu cha kusini cha Kyushu.

Picha za video katika televisheni ya Taifa ya Japan, NHK, zilionyesha miti ikitikisika kwa nguvu kutokana na kimbunga, huku mvua zikinyesha kwa nguvu katika vibaraza pembeni ya barabara. Nyumba ya kuotesha maembe katika kisiwa cha Ishigaki kiliharibiwa. Katika kisiwa kikuu cha Okinawa, wazee wawili walianguka na kujeruhiwa kidogo, kulingana na taarifa za vyombo vya habari.

Maafisa wanasema kusogea polepole kwa kimbunga hicho kunaweza kuongeza kiwango cha mvua na hatari ya kuwepo mafuriko katika mji wa kusini ambapo mawingu maziko yametanda.

Nchini Taiwan, zaidi ya wakazi 600 huko katika kaunti za New Taipei, Taoyuan na Hsinchu waliondolewa na kupelekwa maeneo salama Jumamosi wakati mvua kubwa na upepo wenye kasi ukipiga, kulingana na Shirika la habari la Central News la kisiwa hicho.

Kimbunga hicho kilisababisha maporomoko ya ardhi katika kaunti ya Miaoli na kuangusha miti zaidi ya 100 iliyoko pembeni mwa barabara. Takriban safari 40 za ndege na zaidi ya huduma 100 za feri kote nchini Taiwan zilisitishwa Jumamosi.

XS
SM
MD
LG