Kimbunga hicho kilipita Madagascar Januari 22, na kuongeza siku za mvua kubwa. Nchi hiyo ilitangaza hali ya maafa Alhamisi usiku, ikiripoti kuongezeka kwa idadi ya vifo kutoka na Ana kufikia 48, watu waliouawa na maporomoko ya ardhi na majengo yaliyoanguka au kusombwa na maji.
Kisha kimbunga Ana kilielekea Msumbiji Januari 24, ambapo watu 18 wameripotiwa kufariki, kabla ya kuingia Malawi, ambako kilisababisha kukatika kwa umeme. Idadi ya vifo vya Malawi iliongezeka hadi 20 siku ya Alhamisi.
Katika mataifa yote matatu, Ana ameathiri mamia kwa maelfu ya watu na kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.