Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:56

Madagascar, Msumbiji na Malawi waeleza vifo kutokana na kimbunga Ana vimefikia 70


Watu wakitembea katika barabara iliyofurika maji ya mafuriko huko mji waChikwawa, Malawi, Jan. 25, 2022.
Watu wakitembea katika barabara iliyofurika maji ya mafuriko huko mji waChikwawa, Malawi, Jan. 25, 2022.

Serikali na maafisa wa idara za dharura huko Madagascar, Msumbiji na Malawi wametangaza Alhamisi kwamba idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Ana imeongezeka na kufikia 70.

Maafisa wa serikali hizo wanasema wangali wanatathmini hasara zilizotokana na mvua nyingi zilizoanza tangu wiki iliyopita kabla ya kimbunga kupita katika bahari ya hindi kuelekea Malawi.

Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya watu wamekoseshwa makazi katika nchi hizo tatu na wanahitaji msaada wa dharura.

Maafisa wa huduma za dharura wamesema leo kwamba watu 41 wamefariki Madagascar, 18 Msumbiji na 11 Malawi, lakini hakuna aliyefariki Zimbabwe ambayo nayo imekumbwa na mvua nyingi kutokana na kimbunga Ana.

Maelfu ya nyumba na miundo mbinu imeharibika na idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa, OCHA, inasema watu 110,000 katika wilaya 6 za kati za Madagascar pamoja na mji mkuu wamelazimika kuhama makazi yao.

Mwanamke akiangalia nyumba yake iliyharibiwa na Kimbunga Ana huko Kijiji cha Kanjedza, Wilaya ya Chikwawa, kusini mwa Malawi, Januari 26, 2022.
Mwanamke akiangalia nyumba yake iliyharibiwa na Kimbunga Ana huko Kijiji cha Kanjedza, Wilaya ya Chikwawa, kusini mwa Malawi, Januari 26, 2022.

Katika mji mji mkuu wa Antananarivuo shule na majengo ya maeneo ya michezo yamegeuzwa kuwa makazi ya dharura ili kuwapatia hifadhi maelfu ya waathirika.

Ravelonorosoa Bernadette ni moja wapo ya waathirika anasema wamepoteza kila kitu.

Ravelonorosoa Bernadette muathiriwa wa mafuriko Madagascar anaeleza: “Nyumba yetu imeharibika kabisa kutokana na mafuriko. Haya ni mafuriko ya pili mwezi huu, mara ya kwanza tulibaki huko lakini safari hii tumelazimika kuondoka hatuna mahala pakulala na mtoto wetu ni mgonjwa”

Maafisa wa serikali ya Madagascar wanasema idadi ya waliofariki na kujeruhiwa huenda ikaongezeka kutokana na nyumba nyingi za udongo kuporomoka na watu kukwama ndani ya vifusi.

Rakotoniaina Nathalie ni muathiriwa mwengine katika mji mkuu wa Antananarivo anaeleza: “Rakotoniaina Nathalie, muathirika wa mafuriko Madagascar

Sababu ya sisi kuwepo hapa ni kwamba sehemu ya nyumba yetu imebomoka. Tumeomba msaada tumeletwa hapa. Tukiondoka hapa hatutakua na mahali pa kwenda kuishi.

Umoja wa Mataifa unasema huko kaskazini na kati ya Msumbiji Ana imeharibu zaidi ya nyumba 10,000 shule na hospitali. Idara ya hali ya hewa ya nchi hiyo inasema wanatarajia dhoruba nyingine katika siku zijazo kutokea Bahari ya Hindi na huenda kukawepo vimbunga sita kabla ya kumalizika msimu wa mvua mwezi Machi.

Maafisa wa serikali na Umoja wa Mataifa wanatabiri kwamba hadi watu 500,000 watakuwa wameathiriwa na kinbunga hicho katika majimbo ya Zambezi, Nampula na Sofala nchini Mozambique.

Katika nchi jirani ya Malawi serikali imetangaza hali ya dharura ambako sehemu kubwa ya nchi haina umeme baada ya mafuriko kuharibu vituo vingi vya umema.

Juhudi za uokozi zinaendelea na Mercy Jalilosi na mwenzake Bazilion Benjamin walikuwa garini wanaelekea Blantayre kwa ajili ya kazi wakati gari lao lililposombwa na maji.

Mercy Jalilosi muathiriwa ma mafuriko Malawi anaeleza: Nilianza kuogelea lakini sikujua ninaelekea wapi. Nilijaribu kushikilia mti lakini ukavunjika na hapo nikavutwa na maji. Niliogelea kwa muda mrefu hadi kufikia eleo lililokua na taka nikapumzika na kulala hapo hadi alfajiri. Maji yaliongezeka asubuhi na kusukuma hizo taka kwenye mto huko nikimuomba mwenyezi mungu.

Barabara kuu ya Malawi kuelekea mji mkuu imeharibika na maafisa wa idara ya umeme wanasema wameanza kurudisha umeme kwa sehemu za nchi hii leo.

Umoja wa Mataifa unasema kamba Nchi za Kusini mwa Afrika hasa Msumbiji zimekubwa na dharuba na vyua nyingi zinazoharibu mali mnamo miaka ya hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG