Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:53

Mafuriko ya kihistoria yaua watu 8 New York na New Jersey

Wapita njia wakitafuta hifadhi karibu na eneo la Columbus Circle New York Jumatano, Septemba 1, 2021, wakati athari za Kimbunga Ida kikiendelea kwa kasi kilipokuwa kinapita upande wa ufuko wa bahari Mashariki.(AP Photo/Craig Ruttle)

Mamlaka inasema watu wasiopungua wanane wamefariki huko New York City na New Jersey kutokana na mafuriko ya kihistoria yaliyosababishwa na Kimbunga Ida.

Kimbunga Ida ambacho kilipiga kaskazini mashariki mwa Marekani kwa siku tatu baada ya kuharibu eneo kubwa la kusini mashariki la Louisiana.

Dharuba hiyo ilisababisha mvua nyingi katika Jiji la New York kiasi kwamba Kituo cha Huduma ya Hali ya Hewa ya Kitaifa ilitoa dharura yake ya kwanza ya mafuriko kwa jiji kuu la jirani la Newark, New Jersey.

Magari yakijaribu kupita mitaa iliyojaa maji yakiyakwepa magari yaliyo kwama na kuachwa barabarani huko Teterboro, New Jersey, Alhamisi, Sept. 2, 2021. (AP Photo/Seth Wenig)
Magari yakijaribu kupita mitaa iliyojaa maji yakiyakwepa magari yaliyo kwama na kuachwa barabarani huko Teterboro, New Jersey, Alhamisi, Sept. 2, 2021. (AP Photo/Seth Wenig)

Kituo cha Hali ya Hewa iliweka rekodi ya sentimita 8 za mvua katika hifadhi maarufu ya New York katika saa moja tu, na barabara nyingi ziligeuzwa haraka kuwa mito, na kuacha magari na hata mabasi ya abiria yakizama.

Mfumo wa usafiri wa treni wa jiji ulikuwa umefurika vibaya sana kiasi kwamba Mamlaka ya Usafiri wa mji ilifunga kila kitu isipokuwa moja tu ya safari zake.

Meya wa Jiji la New York Bill de Blasio alitangaza hali ya dharura kwa jiji hilo, pamoja na marufuku ya kusafiri kwa magari yote yasiyo ya dharura hadi saa 11 alfajiri kwa saa za NY, wakati Gavana wa jimbo la New York Kathy Hochul alitoa agizo kama hilo kwa jimbo zima.

XS
SM
MD
LG