Wanaharakati hao ni pamoja na viongozi kama mbunge wa zamani, Cyd Ho, Yeung Sum, Albert Ho na Leung Kwok-hung, anayejulikana kama “long Hair”, na Raphael Wong, Figo Chan, na Avry Ng wa chama cha League of Social Democrats.
Wanaume wote saba walikuwepo mahakamani wakati jaji wa mahakama ya wilaya, Amanda Woodcock, alipowahukumu kwa kushiriki maandamano makubwa hapo Oktoba, mwaka 2019 katika kilele cha maandamano dhidi ya serikali.
Maandamano hayo yalsababishwa na mswaada wenye utata wa uhamishaji watuhumiwa, ambao ulipelekea haja ya kudai uhuru zaidi kwa eneo hilo lenye harakati za kibiashara.
Jaji Woodcock, alisema kuwa wakati katiba ndogo ya Hong Kong, inayojulikana kama sheria ya msingi, inatoa dhamana ya uhuru wa kukusanyika na maandamano, haki hizi sio kamili na zipo chini lakini vinaangaliwa kulingana na masharti ya kikatiba. Hukumu hizo zilianzia miezi 11 hadi 16.