Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:18

Kiongozi wa kumbukumbu ya Tiananmen Square akamatwa Hong Kong

Mwanamke akitoa ishara wakati maafisa wa polisi walipomsimamisha kumpekua Juni 4, 2021, nje ya bostanı ya Victoria Park katika maadhimisho ya 32 ya kamatakamata ya waandamanaji waliokuwa wanaunga mkono demokrasia katika eneo la Tiananmen Square huko Beijing 1989. REUTERS/Lam Yi

Polisi wa Hong Kong mapema Ijumaa wamemkamata kiongozi wa maandamano ya kila mwaka yanayokumbuka msako uliyofanywa na China mwaka 1989 huko Tiananmen dhidi ya wanaharakati wa demokrasia.

Wakati huohuo wakosoaji wa operesheni hiyo wakisema kuwa ukamataji huo ni hujuma kwa matumaini ya demokrasia ya mji huo.

Kukamatwa kwa Chow Hang Tung ambaye ni naibu mwenyekiti wa muungano wa Hong Kong unaounga mkono harakati za demokrasia nchini China, umefanyika wakati maelfu ya maafisa wa usalama wakitarajiwa kwenye eneo la Tiananmen ili kuzuia waandamanaji kukusanyika.

Kumbukumbu hizo ambazo hufanyika Juni 4 kila mwaka kwenye bustani ya Victoria huko Hong Kong ni mojawapo ya ishara ya ari ya watu wa Hong Kong ya kuishi kidemokrasia tofauti na ilivyo China bara.

Chiu Yan Loy ambaye ni mmoja wa viongozi wa muungano wa kidemokrasia amesema kuwa Chow amekamatwa kwa shutuma za kuitisha mkutano usiyo na kibali kwa mujibu wa ujumbe mfupi aliyowaandikia shirika la habari la Uingereza Reuters.

XS
SM
MD
LG