Mkutano huo unalengo la kuwaleta pamoja vongozi wa dunia kujadli mabadiliko ya hali ya hewa, suala ambalo Biden amesema ni kiungo muhimu cha sera za kigeni na usalama wa kitafa wa Marekani.
Maafisa wa Marekani wamesema China ndio mchafuzi mkuu wa gesi ya carbon duniani ikizalisha asilimia 30 ya gesi ya mkaa.
Marekani ni nchi ya pili inayozalisha aslimia 15 na nchi hizi mbili zimetangaza nia ya kupunguza kabisa utowaji wa gesi hiyo kufikia 2050.
Kwa upande mwengine mkutano wa kwanza wa ana kwa ana wa maafisa wa vyeo vya juu wa Marekani na China utafanyika kesho Alhamisi mjini Anchorage Alaska kati ya Mawaziri wa Mambo ya NVje Antony Blinken wa Marekani na Wang Yi wa China.