Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:06

Rais Biden kukutana na wanahabari Machi 25 kwa maswali na majibu


Rais wa Marekani kukutana na wanahabari Machi 25.
Rais wa Marekani kukutana na wanahabari Machi 25.

Rais wa Marekani Joe Biden, atafanya mkutano wake wa kwanza rasmi na wanahabari Machi 25.

Hii ni baada ya kukosolewa kwamba hajakutana na wanahabari mapema kwa ajili ya wasaa wa maswali na majibu.

Msemaji wa White House, Jen Psaki alitangaza tarehe hiyo akiwa Derby, Pennsylvania, huku rais Biden akiwa anatangaza mpango wa afueni ya corona ya trilioni 1.9 katika vitongoji vya mji wa Philadelphia.

Biden amekuwa akitumia muda mchache na wanahabari toka alipoingia madarakani Januari 20, kujibu swali moja ama mawili na kuondoka.

White House imeeleza hatua hiyo kama kuchukuwa tahadhari ya virusi vya corona na kuwa ndiyo sababu ya yeye kufanya hivyo.

XS
SM
MD
LG