Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:40

China : Rais Xi asifia maendeleo yaliyofikiwa na wananchi


Rais wa China Xi Jinping akiwa na Waziri Mkuu Li Keqiang na Rais wa zamani Hu Jintao wakati wa kumalizika kwa maadhimisho ya miaka100 ya kuasisiwa kwa chama cha Kikomunisti katika viwanja vya Tiananmen Square, Beijing, Julai 1, 2021.
Rais wa China Xi Jinping akiwa na Waziri Mkuu Li Keqiang na Rais wa zamani Hu Jintao wakati wa kumalizika kwa maadhimisho ya miaka100 ya kuasisiwa kwa chama cha Kikomunisti katika viwanja vya Tiananmen Square, Beijing, Julai 1, 2021.

Rais Xi Jingping wa China amesifu na kupongeza maendeleo na njia isiyoweza kurudishwa nyuma kutoka kipindi cha kikoloni cha kudhalilishwa hadi kufikia hadhi yake ya taifa kuu.

Akitoa hotuba muhimu kusheherekea miaka 100 tangu kuundwa kwa Chama cha Kikomunist, kiongozi huyo alizungumzia historia ndefu kuanzia masuala mbalimbali ya ndani hadi ya nje na jinsi alivyofanikiwa katika utawala wake mwenyewe.

Akizungumza kwenye uwanja wa Tiananmen ambako muasisi na mwenyekiti mashuhuri Mao Zedong alitangaza kuundwa kwa taifa la Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, Xi alisema enzi ya china kuonewa na kunyanyaswa imekwisha daima akikisifu chama kwa kuongeza mapato ya wananchi, kuleta maendeleo na kudumisha sifa za kitaifa.

Rais Xi : "Tumefanikiwa kukamilisha lengo letu la miaka 100. Jamii ya mapato mazuri ya wastani imeundwa katika ardhi ya China na tumepata ufumbuzi wa kihistoria katika kutanzua kabisa tatizo la umaskini."

Xi ambaye pia ni mwenyekiti na rais wa kamati kuu ya jeshi akiwahutubia watu 72,000 waliohudhuria sherehe hizo amewataka Wachina ndani na nje ya nchi kuungana pamoja kwa kutumia ubunifu wao na nguvu zao zote kufikia lengo la pamoja la kuimarisha maslahi ya taifa na kuendelea mbele kuleta ustawi zaidi wa jamii.

Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 100 wakinyanyua bendera zao.
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 100 wakinyanyua bendera zao.

"Katika safari mbele yetu inatubidi kuhakikisha umoja wetu na kuimarisha mungozo wa kisaisa na kupanua maridhaino kwa kuwaleta pamoja wenye maarifa ya juu na kupanua maslahi yetu ya pamoja," amesema Xi.

Rais Xi alizungumzia ufanisi wa kiuchumi, kibiashara na kijeshi akisisitiza kwamba wataendelea na imani ya dhati chini ya msingi wa nchi moja mifumo miwili, ambapo wananchi wa Hong Kong, na wananchi wa Macao wanaendelea kuwa na mamlaka yao ya ndani. Lakini amesisitiza kwamba serikali kuu ina mamlaka kamili ya kisheria katika maeneo hayo mawili ili kulinda maslahi ya usalama wa kitaifa.

Leo vile vile ni miaka 24 tangu Uingereza, mtawala wa zamani wa kikoloni wa Hong Kong ilikabidhi mamlaka kwa Bejing, siku ambayo siku za nyuma kulikuwa na maandamano makubwa ya kutetea demokrasia, lakini mwaka huu polisi wamezuia aina yeyote ya mandamano.

Wakati huohuo alizungumzia juu ya kutanzua suala la Taiwan na kutekeleza malengo ya china kuungana tena.

Wakati huohuo rais Xi alitoa matamshi ya kukaidi hatua za wahasimu wake wa kigeni wakiongozwa na Marekani akifufua hisia za kizalendo na akijisifia kama bingwa na mtetezi wa hadhi mpya ya china.

Chama cha Kikomunisti cha China - CPC kikiadhimisha miaka 100 tangu kuundwa kwake mwaka 1921 kina wanachama zaidi ya milioni 95 na ni chama kikuu cha kisiasa duniani.

Vyanzo vya Habari : AFP/ AP

XS
SM
MD
LG