Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:37

UN yatoa wito kuongezwa haraka misaada ya kibinadamu na fedha Msumbiji


 Antonio Vitorino
Antonio Vitorino

Shirika la Umoja wa Mataifa, UN, la uhamiaji, IOM, limetoa wito wa upanuzi wa haraka wa misaada ya kibinadamu na fedha zaidi kwa ajili ya operesheni katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado nchini Msumbiji.

Antonio Vitorino, mkurugenzi wa IOM anayeitembelea Msumbiji amesema Jumatano msaada unahitajika kuwasaidia maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kwa sababu ya ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Amesema ufadhili zaidi unahitajika kwa ajili ya misaada ya kibinadamu inayohitajika kuokoa maisha na kufanya kazi kwa ajili ya kufikia suluhisho la kudumu, hasa kabla ya kipindi kingine cha mvua na kimbunga mwezi Disemba.

Mkuu huyo wa IOM ametembelea wilaya za Metuge ambazo zinahifadhi watu takriban 125,000 kati ya zaidi ya laki nane waliokoseshwa makazi tangu mwishoni mwa mwaka 2017.

Hata hivyo IOM imesema imetoa msaada kwa zaidi ya watu laki sita huko Cabo Delgado kati ya mwezi januari na julai ikiwemo ujenzi wa makazi na kutoa vifaa vya nyumbani.

XS
SM
MD
LG