Botswana ilituma wanajeshi nchini Msumbiji siku ya Jumatatu, na kuwa nchi ya kwanza kati ya mataifa wanachama 16 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kupeleka wanajeshi kusaidia kupambana na uasi wa Waislamu wenye itikadi kali katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.
Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi, alisema wanajeshi watashirikiana na vikosi vya jeshi la Msumbiji na wanajeshi wengine waliopelekwa na nchi wanachama wa SADC, ili kumaliza uasi ambao zaidi ya watu 3,000 wamekufa tangu mwaka 2017.
Vikosi vya Botswana vitajiunga na wanajeshi 1,000 waliowasili Msumbiji mapema mwezi huu kutoka Rwanda, ambayo si mwanachama wa SADC. Wanajeshi wa Rwanda waliripoti tayari kuwa katika operesheni, tovuti ya habari ya ndani Carta de Moçambique ilisema walikuwa wamewaua waasi 30 wiki iliyopita.
Ujumbe wa SADC nchini Msumbiji utaongozwa na Jenerali wa Afrika Kusini Jenerali Xolani Mankayi, ambaye yuko Msumbiji kama ni sehemu ya waliopelekwa mapema.