Nyusi alikuwa akilihutubia taifa kuhusu mzozo uliopamba moto wakati waasi wakishambulia mji wa pwani wa Palma mwezi March, karibu na miradi ya gesi yenye thamani ya dola billioni 60 ambayo ilikua inalenga kubadilisha uchumi wa Msumbiji.
Akitoa hotuba hiyo kupitia televisheni na mitandao ya kijamii, Nyusi ametangaza kwamba wanajeshi wa SADC wanahamasishwa kuingilia kijeshi katika mkoa wa Cabo Delgado, ulioko chini ya uasi wa kijihadi.
Ombi la SADC kuingilia kati huko Cabo Delgado limekamilishwa rasmi, waziri wa ulinzi wa Msumbiji, Jaime Neto ameliambia shirika la habari la AFP, kwa njia ya simu.