Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:16

Watu wa kaskazini mwa Msumbiji wapo hatarini na njaa


Takriban watu milioni moja wanakabiliwa na baa la njaa kaskazini mwa Msumbiji, ambapo maelfu ya watu wamekimbia maeneo yao kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wenye msimamo mkali.

Shirika la umoja wa mataifa la chakula (WFP) limeeleza.

Wanamgambo wenye uhusiano na Islamic State mwezi uliopita walishambulia mji wa Palma, uliopo katika jimbo la Cabo Delgado karibu na miradi ya gesi iliyo chini ya makampuni makubwa ya mafuta ikijumuisha Total na Exxon.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba shirika la mpango wa chakula (WFP) limeeleza katika mkutano na wanahabari mjini Geneva kwamba watu 950,000 wanakabiliwa na njaa nchini Msumbiji.

Imetoa mwito kwa wafadhili kuchangia dola milioni 82 kukabiliana na hali hiyo. Msemaji wa (WFP) Kaskazini mwa Msumbiji, Tomson Phiri, amesema kwamba familia na watu ilibidi wakimbie na kuacha vitu vyao pamoja na maisha yao ili kutafuta usalama.

XS
SM
MD
LG