Kamanda wa jeshi Cristo-vao Chume amesema wengi wa waliookolewa ni wanawake na watoto, na kwamba wamekabidhiwa kwa serikali kwa usaidizi zaidi.
Kamanda huyo amesema wanamgambo wanaendelea kuwepo,katika wilaya ya Palma ingawa usalama wa eneo hilo unasemekana umedhibitiwa.
Jenerali huyo amesema wanamgambo wanaendelea kuteketeza nyumba katika baadhi ya vijiji.
Aliwashutumu wanamgambo hao kwa kutumia raia kama ngao jambo ambalo amesema linazifanya operesheni za kijeshi kuwa ngumu.
Serikali ilisema Jumanne vikosi vyake viliwaua zaidi ya waasi 150 katika wilaya ya Palma kati ya tarehe 21 na 23 Juni.
Katika siku za hifi karibuni jeshi la Msumbiji limeongeza juhudi zake katika vita dhidi ya wanamgambo katika jimbo hilo.