Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:17

Timu ya Msumbiji yarejesha matumaini kwa ushindi wa pointi 88-74


Ferroviario de Maputo ikichuana na AS Douanes Kigali, Rwanda, katika Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika (BAL) Mei 19, 2021.
Ferroviario de Maputo ikichuana na AS Douanes Kigali, Rwanda, katika Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika (BAL) Mei 19, 2021.

Baada ya kufungwa katika mchezo wao wa ufunguzi Jumatatu, timu ya Msumbiji ya Ferroviario de Maputo imerejesha matumaini katika ligi ya Basketball kwa ushindi wa pointi 88-74 dhidi ya AS Douanes ya Senegal mjini Kigali Rwanda.

Ferroviario iliongoza toka mchezo kuanza lakini timu ya Senegal kwa Haraka ilianza kurejea mchezoni kwa pointi tatu ya Cheikh Bamba Diallo, na danki la Hassan Ahmed Elsayed.

Mchezaji wa ASDouanes, Mamadou Lamine Diop alifunga pasi iliyorudi baada ya kuzuiwa na Adjehi Baru wa Ferroviario.

Diop aliendelea na pointi tatu, na kufanya pointi za mchezo kuwa 42-41, lakini Myck Kabongo wa Maputo alijibu kwa pointi tatu.

Mruko wa Diop uliiweka AS Douanes mbele, na kuifanya timu yake kuendelea kuongoza kwa danki baada ya pasi iliyotolewa na Christopher Jarrod Cokley.

Lakini Ferroviario iliendelea kukaribia baada ya pointi tatu za Alvaro Masa ambaye alikuwa mchezoni dakika chache baadaye kwa kufunga baada ya kirushwa pointi tatu.

Pointi tatu zilizo rushwa na Masa pembeni mwa goli, kulifanya Maputo kuongoza Mapema katika robo ya nne. Dermacus Holland aliongeza pointi tatu nyingine na Maputo ikaendelea kuongoza.

Alvaro Masa ambaye alimaliza mchezo kwa pointi 26, rebounds 9, na kutoa pasi mara 4, kulifanya mchezo kuondoka kwa AS Douanes, hasa kwa pointi tatu nyingine na kuipatia timu ya Maputo ushindi wa kwanza katika mashindano hayo.

Mamadou Faye aliandikisha pointi 21, kudaka mpira mara 4, na kutoa pasi mara 5 licha ya juhudi kushindwa kuifanya AS Douanes.

XS
SM
MD
LG