Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:44

Katibu Mkuu wa UN akumbusha jukumu la kimataifa kusaidia wakimbizi


Watoto wakicheza pamoja katika kambi ya wakimbizi katika Kituo cha Makaribisho cha Hamdayat katika jimbo la Gedarif.
Watoto wakicheza pamoja katika kambi ya wakimbizi katika Kituo cha Makaribisho cha Hamdayat katika jimbo la Gedarif.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN, Antonio Gutteres anatukumbusha mwaka huu 2021 kwa pamoja pekee yake tutaweza kutokomeza janga la COVID-19 na kufufua tena maisha na uchumi wetu. 

Kwa hivyo anasema tukishirikiana pamoja licha ya changamoto zilizopo tutaweza kuwasaidia wakimbizi na waliokoseshwa makazi kuchagia katika dunia iliyo salama, yenye nguvu na inayostawi zaidi.

Guterres alisema hayo katika kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani tarehe 20 Juni.

Kutokana na hayo kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwashirikisha na kuwapokea wakimbizi katika nyanja zote ikiwa ni mfumo wa elimu, afya, shule na michezo.

Na Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR, linasema kwa pamoja tutapata afweni, tutajifunza na kunawiri.

Kamishna mkuu wa UNHCR Filippo Grandi akishiriki kwenye mkutano wa UN kuzindua wiki ya wikimbizi kupitia mtandao tarehe 16 Juni 2021, amesema haitoshi tu kuwahusisha wakikmbizi kwenye mifumo ya elimu na afya lakini kuna mambo mengi nyeti yanayo hitajika

Filippo Grandi
Filippo Grandi

“Kuwapatia hifadhi ni utaratibu wa kisheria katika nchi, ni kupewa hati za kuishi, kuweza kuwa na akaunti ya benki na nina dhani ilitajwa hapa, kuweza kupata mawasiliano ya mtandao. Mambo haya huenda yasiwe muhimu na kwa hakika ni mambo tunayaofanya kwa kawaida kila siku bila ya kutilia maanani lakini, ikiwa huna mambo hayo yote ambayo ni ngumu kwa wakimbizi kupata basi hakuna matumaini ya kuhusishwa kikamilifu katika jamii. Huna vifaa vinavyohitajika kwa maisha ya kawaida,” Amesema Guterres.

Hali hiyo ndiyo inawakabilia karibu watu milioni 82.3 kote dunaini waliokoseshwa makazi wakiwemo wakimbizi milioni 26.4, miongoni mwao wapalestina milioni 5.7 kulingana na takwimu zilizotolewa na ripoti mpya ya UNHCR siku ya Ijumaa June 18, 2021.

Ripoti inaeleza kwamba kwa siku watu elfu 42 500 wanakimbia kutoka makazi yao wakitafuta hifadhi na mwaka jana pekee ni watu milioni 13.9 waliokoseshwa makazi duniani.

Ripoti inasisitiza kwamba cha hatari ni kuwa asilimia 42 ya watu waliokoseshwa makazi ni wasichana na wavulana chini ya miaka 18. Na hadi hii leo Wasyria milioni 11 hawana makazi wakiwa ndio idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi moja.

Kinachoshangaza watayarishaji wa ripoti wanasema ni kwamba idadi ya waliokoseshwa makazi na kubaki ndani ya nchi zao imefikia milioni 48 mwaka 2020, kutokea milioni 2 miaka 10 iliyopita.

Linda Thomas-Greenfield
Linda Thomas-Greenfield

Takwimu hizo zilitajwa pia kwenye mkutano huo wa UN wiki hii uliyohudhuriwa pia na balozi wa marekani kwenye UN Linda Thomas Greenfield. Alitoa wito kwa dunia kuwakumbuka hasa wakimbizi wa Syria akitaja kuwa ni mzozo mbaya kabisa wa kibinadamu hii leo duniani.

“Tunaposherekea nguvu za kumhusisha kila mmoja na kutoa heshima kwa wakimbizi Juni 20 hebu tuwakumbuke mamilioni ya Wasyria kote duniani wanaohitaji sana tena sana msaada wetu. Wao na mamilioni ya wengine kote duniani wanaotutegemea. Wanatutegemea kuwasaidia kuokoa maisha yao. Wanategemea hisani na ubinadamu kuwanyooshea mkono wakati huu wakiwa katika maisha ya hatari wakihitaji msaada,” amesema Thomas-Greenfield.

Thomas-Greenfield anasema anaona fahari kusema kwamba Rais Joe Biden tangu siku ya kwanza kuchukua madaraka amehakikisha kwamba Marekani inabaki kuwa nchi yenye dhamira ya kuwapatia msaada na usalama wale waliyo hatarini.

Mkuu wa UNHCR anasema cha ajabu na kusikitisha ni kwamba wakati wa janga la Covid 19 kila kitu kilisita kuanzia uchumi biashara na kazi zote kufungwa lakini, mapigano ghasia na mauaji yameendelea.

“Na bila shaka Ethiopia ambako mzozo wa Tigray umezusha hali mpya na hata sasa hatuna hakika idadi yao huenda ikafikia milioni moja zaidi ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao na karibu elfu 50 hadi elfu 60 wamevuka mpaka na kuingia Sudan,” Ameesema Grandi.

Kwa mwaka uliyopita mizozo mikubwa iliyoongeza wakimbizi kulingana na ripoti hiyo mpya zaidi ilikuwa Yemen, Ethiopia katika jimbo la Tgray, Msumbiji, Venezuela na Myanmar.

Grandi anasema muelekeo wa watu wanaokoseshwa makazi mwaka 2021 sio nzuri hata kidogo. Mnamo miezi sita ya kwanza ya mwaka huu anasema ni wakimbizi wachache waliorudi nyumbani na mzozo wa kutanzua hali ya wakimbizi umekwama.

XS
SM
MD
LG