Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:07

Marekani yatoa msaada kwa jeshi la Msumbiji


Wanajeshi wa Msumbiji waliopatiwa mafunzo na Marekani huko Msumbiji, Juni, 2021
Wanajeshi wa Msumbiji waliopatiwa mafunzo na Marekani huko Msumbiji, Juni, 2021

Kama sehemu ya ushirikiano wa Marekani na Msumbiji, wanajeshi 40 wa Msumbiji na madaktari walimaliza programu mbili za mafunzo juu ya mbinu za dharura za kuokoa maisha kwenye uwanja wa vita. Mafunzo ya Tactical Combat Care (TCCC) na Combat Lifesaver (CLS) yataboresha moja kwa moja kiwango cha kuokoa maisha ya wanajeshi wa Msumbiji katika vita.

Programu ya TCCC iliwapatia mafunzo wafanyakazi wa huduma 26 juu ya huduma ya matibabu ya dharura, madaktari na wauguzi wakati wa mizozo. Katika mpango wa CLS, wanajeshi 14 kutoka matawi yote ya jeshi la Msumbiji walijifunza jinsi ya kutoa msaada wa dharura kwa wanajeshi wenzao waliojeruhiwa.

Mafunzo hayo yatawawezesha wanajeshi wa Msumbiji na wataalamu wa matibabu kutibu majeraha na kuzuia kutokwa na damu nyingi, sababu inayoongoza ya kifo katika uwanja wa vita. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilifadhili program hizo mbili, pamoja na dola 730,000 katika vifaa vya mafunzo ili kuruhusu waalimu wapya wa Msumbiji kufundisha kozi hiyo kote nchini.

XS
SM
MD
LG