Idadi ya vifo kutokana na kimbunga Rai, kilichopiga Ufilipino wiki iliyopita, imevuka watu 200.
Wafanyakazi wa kutoa misaada wameripoti kwamba uharibifu mkubwa umetokea katika sehemu za pwani ambapo nyumba, hospitali na shule viliharibiwa vibaya.
Msemaji wa polisi amewaambia waandishi wa habari kwamba karibu watu 208 wamethibitishwa kufariki, na 52 hawajulikani walipo.
Kimbunga hicho kilipiga majimbo ya kati na kusini mwa Ufilipino wiki iliyopita.
Zaidi ya nusu ya vifo vilivyoripotiwa na polisi, vipo katika eneo la Visayas, lenye mikoa ya Bohol ambapo ni kitovu cha shughuli za utalii.
Shughuli za kutoa misaada zinaendelea lakini zinaathiriwa na uharibifu uliotokea kwa mfumo wa mawasiliano na umeme.