Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:03

Kimbunga Gombe chagonga Msumbiji


Athari za kimbunga nchini Msumbiji kwenye picha ya awali
Athari za kimbunga nchini Msumbiji kwenye picha ya awali

Kimbunga Gombe kimepiga kaskazini mwa Msumbiji mapema Ijumaa wakati kiakiambatana na mvua kubwa pamoja na upepo mkali na  kusababisha uharibifu mkubwa kwa nyumba na miundo mbinu pamoja na kifo kimoja shirika la habari la AP limeripoti.

Kulingana na walioyshuhudia, kimbunga hicho ambacho ni moja ya vingi vilivyopiga taifa hilo katika siku za karibuni kutoka bahari hindi na cha hivi karibuni na kimepiga jimbo la Nampula Ijumaa asubuhi kimeangusha miti pamoja na kuezua mapaa ya nyumba.

Televisheni ya taifa hilo ya Miramar imesema kwamba mkazi mmoja ameuwawa na umeme wakati akijaribu kuokoa paa la nyumba yake kutokana na kimbunga hicho. Ripoti zinaongeza kusema kwamba huduma muhimu kama vile umeme, maji na simu zimekatika. Idara ya kitaifa ya majanga imesema kwamba shughuli za upelekaji misaada pia zimeathiriwa kutokana na kuharibiwa kwa ghala zinazohifadhi misaada .

XS
SM
MD
LG