Takriban watu 14 wameuawa nchini Madagascar wiki hii na dhoruba ya kitropiki ya Dumako, shirika la kusughulikia misaada ya maafa la serikali lilisema, wakati kisiwa hicho kikijiandaa na kimbunga kingine kinachotarajiwa kupiga Jumanne.
Takriban watu 4,323 walilazimika kuhama makazi yao wakati Dumako ilipotua mashariki mwa nchi hiyo siku ya Jumanne, shirika la maafa lilisema Ijumaa. Walikuwa wamepatiwa hifadhi katika maeneo 12.
Taifa la kisiwa cha Bahari ya Hindi linapitia msimu wake wa dhoruba. Jumla ya watu 124 walifariki mwezi huu wakati kimbunga cha kitropiki cha Batsirai kilipiga pwani ya kusini mashariki mwa kisiwa hicho.
Kimbunga kingine, Emnati, kinatabiriwa kupiga karibu na eneo hilohilo lililoathiriwa na Batsirai, alisema Nomen-janahary Mamy Andria-mirado, mtabiri wa hali ya hewa katika idara ya taifa ya hali ya hewa.