Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:01

Kimbunga Emnati chaongeza uharibifu Madagascar

FILE PHOTO: Athari za kimbunga Batsirai Madagascar.
FILE PHOTO: Athari za kimbunga Batsirai Madagascar.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba jamii ambazo ziliathiriwa na kimbunga Batsirai kilichopiga kisiwa hicho mapema mwezi huu, huenda zikaathirika kwa mara nyingine tena.

Kimbunga Emnati kimepiga sehemu za kusini mashariki mwa Madagascar Jumanne usiku na kuongeza uharibifu kwenye kisiwa hicho ambacho tayari kimeharibiwa na vimbunga.

Kimbunga Emnati kimekuwa na upepo wa kasi ya kilomita 135 kwa saa.

Ni tukio la tano la hali mbaya ya hewa, na dhoruba ya nne kupiga kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi katika muda wa mwezi mmoja.

Dhoruba zilizopiga awali zilisababisha maelfu ya watu kukosa makazi na mamia kuuawa tangu katikati ya mwezi Januari.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba jamii ambazo ziliathiriwa na kimbunga Batsirai kilichopiga kisiwa hicho mapema mwezi huu, huenda zikaathirika kwa mara nyingine tena.

Maafisa wana wasiwasi kwamba mvua nzito, mafuriko na upepo mkali huenda vikasababisha uharibifu mkubwa.

Mataifa ya kusini mwa Afrika ya Malawi, Msumbiji, na Zambia yamekuwa yakishuhudia hali mbaya ya hewa kutokana na Dhoruba Dumako iliyopiga sehemu hiyo wiki moja iliyopita.

XS
SM
MD
LG