Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:48

Bobi Wine adai anahisi yuko kizuizini nyumbani kwake


IMbunge Robert Kyagulanyi
IMbunge Robert Kyagulanyi

Mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi amesema ataomba kibali kutoka polisi cha kuitisha maandamano Jumanne kupinga hatua ya polisi ya kuzuia tamasha lake lisifanyike Jumatatu.

Iwapo Jeshi la Polisi litakataa kumpa kibali, amesema ataitisha maandamano nchi nzima kupinga hatua hiyo ya polisi kumzuia kufanya matamasha yake.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa Bobi Wine tayari alikuwa amekwisha fungua kesi mahakamani kupinga hatua hiyo. Pia mapema mwaka 2019 alipeleka madai yake katika Tume ya Haki za Binadamu ya Taifa ya Uganda.

Wakati huohuo kiongozi wa upinzani Dkt Kiiza Besigye, amekuwa akijikuta katika mivutano na maafisa wa polisi takriban mwezi mzima sasa.

Besigye, ambaye amekuwa akifanya ziara kote Uganda kukutana na wafuasi wake pamoja na viongozi wa chama cha Forum for democratic forces, FC, amekuwa akizuiliwa kufanya mahojiano na vyombo vya habari hasa radio, na radio hizo kuzimwa.

Besigye, amesikika mara kadhaa akisema kwamba wakati umefika wa kumwondoa rais Yoweri Museveni kwa kutumia nguvu za wananchi.

Kuhusu kadhia ya Bobi Wine taarifa zinaeleza kuwa Bunge lilikuwa limetoa maelekezo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu likiwataka polisi kuacha mara moja kumzuia Bobi Wine kufanya maonyesho ya matamasha yake. Lakini amri hiyo ya bunge ilipuuzwa na jeshi la polisi.

Mpaka sasa mwanamuziki huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi hajaweza kufahamu iwapo yuko kizuizini nyumbani kwake akisema kupitia akaunti yake ya Tweeter kwamba wanaokuja kumuona nyumbani hapo wanapekuliwa na polisi wanapoingia na kutoka.

Mapema Jumatatu jeshi la polisi lilimkamata na haikujulikani amepelekwa wapi, baada ya kuwepo mvutano kati yake na polisi waliofutilia mbali tamasha lake la muziki liliokuwa lifanyike sikukuu ya Pasaka.

Wakati wakimkamata polisi walitumia nguvu kulifungua gari ambalo mbunge huyo alikuwa ndani yake kabla ya kuvunja vioo vyake na kumtoa nje.

Hata hivyo mwanamuziki Nubian Li ambaye alikuwa akiandamana naye katika gari hilo hakukamatwa.

Wakati akikamatwa hali haikuwa shuwari kufuatia kitendo cha polisi kuzuia msafara wa mwanamuziki huyo wa kizazi kipya maarufu kama Bobi Wine. Mbunge huyo alikuwa anaelekea katika tamasha lake la One Love huko Busabala.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor nchini Uganda Mbunge wa Makindye Magharibi Allan Ssewanyana alizirai na ikalazimika wafuasi wake kumbeba hadi katika gari moja ambalo lilikuwa likimsubiri.

Ripoti zaidi zinaelezea kuwa waandalizi wa tamasha hilo la Bobi Wine nao pia wamekamatwa.

Hatua hii ya polisi inatokana na kauli ya Rais Yoweri Museveni kuwa hatokubali matamasha ya muziki uliojaa siasa na kuonya hakuna mtu atakayefidiwa kwa matamasha ambayo yamezuiliwa kufanyika.

Museveni aliyasema hayo katika mkutano wa wanachama na mapromota wa muziki nchini Uganda pamoja na wamiliki wa maeneo yanaopigwa muziki Ikulu na alitoa shilingi bilioni mbili za Uganda kufidia hasara waliopata baada ya maafisa wa polisi kufuta matamasha ya muziki wa Bobi Wine.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG