Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:14

Hatimaye Bobi Wine aruhusiwa kuondoka Uganda


Bobi Wine akipandishwa kwenye gari ya kubeba wagonjwa.
Bobi Wine akipandishwa kwenye gari ya kubeba wagonjwa.

Mbunge wa Uganda ambaye inadaiwa aliteswa na maafisa wa usalama ameruhusiwa kusafiri kuelekea Marekani kwa matibabu, mwanaharakati wa kisiasa Uganda ameiambia Sauti ya Amerika.

Kiwanuka Lawrence Nsereko, ambaye anaishi Jimbo la New York, ameiambia Sauti ya Amerika, Ijumaa, kuwa Robert Kyagulanyi ameachiwa huru kutoka Hospitali ya Kampala ambako alikuwa anashikiliwa, na kuelekea uwanja wa ndege.

Nsereko amesema alizungumza na familia ya Kyagulanyi muda mfupi baada ya habari za kuachiwa kwake kutangazwa Kampala. Familia yake “inajaribu kuhangaika” kumtafutia usafiri wa ndege, Nsereko amesema. Anavyofahamu ni kuwa Kyagulanyi atakuja eneo la Washington, DC, mara utakapo patikana usafiri.

Alhamisi usiku polisi walimkamata Kyagulanyi na mbunge mwenzake wa upinzani Francis Zaake uwanja wa ndege wa Kampala walipokuwa wanajaribu kutoroka nchini.

Polisi walidai kuwa viongozi hao wa upinzani, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za uhaini walikuwa katika harakati za kukimbia. Hata hivyo Zaake mpaka sasa hajaachiliwa huru.

Watu hao wawili wamesema kuwa waliteswa baada ya kukamatwa huko nyuma, na Hospitali ya Kampala ilitoa pendekezo kwamba wapatiwe matibabu nje ya nchi. Kyagulanyi, mwimbaji maarufu kama Bobi Wine, alikuwa anaelekea Marekani na mwenzake Zaake alikuwa anaelekea India.

XS
SM
MD
LG