Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:16

Polisi wafunguka juu ya kushikiliwa kwa mlinzi wa Bobi Wine


Wanaharakati nchini Kenya wakiandamana kumuunga mkono Bobi Wine baada ya kuwekwa kizuizini nchini Uganda Agosti 23, 2018.
Wanaharakati nchini Kenya wakiandamana kumuunga mkono Bobi Wine baada ya kuwekwa kizuizini nchini Uganda Agosti 23, 2018.

Polisi wamesema kuwa wanamshikilia mlinzi wa mbunge wa Kyadondo Mashariki, Bobi Wine, Eddie Ssebuufu maarufu kama Eddie Mutwe katika hifadhi iliyo salama mjini Kampala, Uganda.

Msemaji wa Polisi wa eneo la kipolisi la Mjini Kampala, Luke Owoyesigyire, amesema Mutwe yuko kituo cha polisi kilichopo barabara ya Jinja katika hifadhi salama baada ya kupelekwa huko na kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai (CID)

Mutwe inasemekana kuwa alitekwa na watu waliokuwa wamevaa sare za jeshi Agosti 25 kutoka nyumba inayojulikana kama Fire Base (Kikundi cha muziki cha Bobi Wine) kilichoko katika jumba la Ssemakokkiro huko Kamwokya, kitongoji cha Kampala.

“Ninachojua ni kuwa yuko kituo cha polisi cha Jinja katika hifadhi salama chini ya uangalizi wa makao makuu ya CID. Sijui ni makosa gani anachunguzwa kwayo,” Owoyesigyire amesema.

Mutwe alichukuliwa wiki moja baada ya bosi wake kukamatwa na kujeruhiwa na kikosi maalum cha kumlinda Rais Museveni (SFC) kwa tuhuma za kulitupia mawe gari la ikulu wakati wa chaguzi ndogo zilizokuwa zikifanyika Manispaa ya Arua.

Hapo awali polisi na jeshi walikanusha kuwa wanajua alipo Mutwe kwa kipindi cha wiki mbili mpaka pale Mahakama Kuu Kampala, ilipo amrisha mkuu wa usalama jeshini (CMI), Mwanasheria Mkuu na Mkuu wa Majeshi wamlete mara moja Mutwe mahakamani.

Amri ya mahakama ilitokana na ombi la kisheria, kutoka kwa wakili wake alilowasilisha mahakamani, ikiwa ni ombi maalum ( habeas corpus) kwa mahakama kuamuru mtu aliyewekwa kizuizini kuletwa mbele ya jaji au hakimu hususan kumwezesha mtu huyo kuachiwa kutokana na kuzuiliwa bila ya uhalali wowote.

Kupitia wakili wake Anthony Kusingura wa kampuni ya mawakili ya Kiiza Mugisha, Mutwe aliiomba Mahakama Kuu kuwa iamuru CMI na Mwanasheria Mkuu kumleta mahakamani Mutwe mara moja.

XS
SM
MD
LG