Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:37

EU yataka Uganda iwawajibishe maafisa wa usalama


Bunge la Umoja wa Ulaya
Bunge la Umoja wa Ulaya

Bunge la Umoja wa Ulaya linataka vyombo vya usalama nchini Uganda kuacha kutumia nguvu kupita kiasi wakati wanapo kabiliana na wanasiasa wanaoipinga serikali.

Bunge ambalo ni mfadhili mkuu wa Uganda limejadili hali ya kibinadamu nchini Uganda, na kutaka maafisa wote wa usalama walio husika katika kuwapiga wabunge Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine na Francis Zaake miongoni mwa wengine, pamoja na kuwaua wafuasi wao, kukamatwa na kushtakiwa mara moja.

Hata hivyo, halijatoa masharti yoyote endapo maafisa husika hawatakamatwa.

Bunge hilo limesisitiza kwamba ni muhimu kwa raia wa Uganda na washirika wake kuheshimu mfumo wa demokrasia na uhuru wa watu, ikiwemo kuheshimu bunge na wabunge.

Kauli ya Museveni

Hata hivyo, Museveni anadai kwamba wabunge wa upinzani, wanapewa ufadhili na serikali za nje yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, kuitatiza serikali yake kwa kufanya maandamano.

Serikali ya Uganda, mara kadhaa, imekana madai ya maafisa wake wa usalama kuwatesa washukiwa wakiwa kizuizini na badala yake kusema kwamba wanaodai kupigwa na kuumizwa ni waongo.

Bunge la EU pia linataka maafisa wa usalama wanao wapiga waandishi wa habari kukamatwa na kushtakiwa nchini Uganda.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG