Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:22

Serikali ya Uganda yakanusha Bobi Wine hakuteswa


Bobi Wine
Bobi Wine

Serikali ya Uganda imemjibu mbunge Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ikikanusha madai yake kuwa alipigwa na kuumizwa na walinzi wa kikosi maalum cha Rais Yoweri Museveni (SFC).

Naibu msemaji wa serikali ya Uganda, Kanali Shaban Bantariza, amesisitiza Ijumaa kwamba hakuna dhuluma za aina yoyote alizo fanyiwa Bobi Wine na kwamba nia yake ni kuchafua sifa ya serikali, kimataifa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:36 0:00

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti kuwa katika kikao na waandishi wa habari Washington, Marekani, Alhamisi, Bobi Wine alielezea kipigo alichopata kutoka kwa wanajeshi na kuonyesha vidonda mwilini mwake vinavyoonekana kuanza kukauka kutokana na matibabu anayopata.

Bobi Wine, ametupilia mbali taarifa ambayo imetolewa na serikali ya Uganda kwamba nia yake ni kusababisha vurugu nchini mwake, akisisitiza kwamba analofanaya ni kupigania uhuru na haki ya kila mtu, katika mazingira yanayoheshimu haki za kibinadamu na demokrasia.

Hata hivyo, Bobi amesema kwamba amelazimika kuongea na waandishi wa habari kwa sababu dunia inataka kujua mengi yaliyomfika na kusema kwamba punde tu atakapomaliza matibabu na ukaguzi wa madaktari, atarejea nchini mwake.

Mbunge mwingine Francis Zaake, aliyepigwa siku moja na Bobi Wine, anatibiwa nchini India, wakati ikiripotiwa kuwa hali yake ya kiafya ni mbaya.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG