Watu 3 akiwemo Mmarekani wauawa kwa kuchomwa visu Uingereza

Polisi wakiimarisha ulinzi katika mji wa Reading, England, Jumapili June 21, 2020 baada ya watu watt kuuawa kwa kuchomwa visu.

Mwanaume wa Kimarekani ni kati ya watu watatu waliouawa kwa kuchomwa visu katika mji wa Reading nchini Uingereza Jumamosi, balozi wa Marekani nchini Uingereza amethibitisha tukio hilo Jumatatu, bila ya kutaja jina la raia huyo.

Balozi Woody Johnson ametuma ujumbe wa tweet akitoa “rambirambi zake za dhati kwa familia ya wale wote waliouawa katika shambulizi hilo la Juni 20”, akiongeza kuwa mmoja wa waliokufa ni raia wa Marekani.

“Sikitiko letu liko kwa wote walioathirika na tukio hili,” Johnson ameandika. “Tunalaani vikali shambulizi hili na tumetoa msaada wetu kwa vyombo vya usalama vya Uingereza.”

Jeshi la polisi Uingereza limesema raia mwanaume mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa katika eneo la tukio na inaaminika alikuwa amefanya shambulizi hilo peke yake, tukio hilo linashughulikiwa kama linahusika na ugaidi, hivi sasa linachunguzwa na kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi.

Watu wengine watatu walikuwa wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo katika uwanja wa Bustani ya Forbury mjini Reading, mji wenye watu 200,000, ulioko kilomita 65 magharibi mwa London.

Gazeti la Philadelphia Inquirer limemtaja Mmarekani aliyeuawa kama Joe Ritchie-Bennett, umri miaka 39, ambaye alihamia Uingereza takriban miaka 15 iliyopita.

Gazeti hilo limemnukuu baba yake, Robert Ritchie, akisema kuwa hapo awali mtoto wake alikuwa akifanya kazi

katika kampuni ya mawakili London na katika kipindi cha miaka 10 iliyopita alikuwa ameajiriwa na kampuni ya madawa ya Dutch pharmaceutical iliyo na makao ya makuu mjini Reading.